Wabunge wawekewe KPI's | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wawekewe KPI's

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkere, Aug 13, 2010.

 1. M

  Mkere New Member

  #1
  Aug 13, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi si mpenzi sana wa siasa wala si mwanachama wa chama chochote na nilipiga kura nilipokuwa na miaka 18 miaka 20 iliyopita na nilipiga kwa vile nilitaka kujaribisha ila sijaona cha mabadiliko yoyote kwa kweli ndio maana huwa sihangaiki kwenda kupanga foleni.

  Katika kipindi hiki cha kutaka mabadiliko kuna wabunge wanaotaka kuingia kuwasilisha majimbo yao na kunawanaotaka kubakia kuendelea kwenda kusinzia bungeni.Mimi binafsi ninaonelea kuwa ni wakati muafaka wa wabunge kufanyakazi kiukweli wawekewe KPI ( Key perfomance indicators) ziwe zinakuwa reviewed kila mwaka na kama hujatimiza malengo kwa asilimia 75% unapigwa chini anachaguliwa mbunge mwingine mwenye ufanisi.
  Nasema hivi kwanini? Sioni sababu ya mtu kuchaguliwa wakati kuna basic things ambazo unaweza kujituma kuvifanya aidha kwa kuhamasisha watu wa jimbo lako au kutafuta misaada mbali mbali kwa wafanya biashara wa eneo lako bila kugonjea serikali. Vitu muhimu kama Zahanati, shule, maji na mambo mengine madogo madogo kwa kweli huwa nasikia uchungu sana kwamba tangu nimezaliwa shida ni zile zile hadi leo hii naelekea uzeeni.
  Kwa wabunge vijana na wazee wa chama chochote kile wekeni KPI's kwa wawakilishi wenu muwa tathmini baada kipindi maalum, laasivyo mtajaza wauza sura, mafisadi, wasinziaji na wahongaji lazima ifikie wakati mtu uchaguliwe kwa ulichofanya tena kwa kiasi kikubwa ili tunapokuchagua tena tunajua tunachagua nini hapo ndio maendeleo yatapatikana wakati wa kubebana umekwisha

  Amani kwenu, mfungo mwema na uchaguzi mwema
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Good idea,

  Tatizo inabidi tuondokane na utamaduni wa "Data Not Available" na tuwe makini sana na jinsi gani hizi data zinapatikana, tusije kupewa data za economic growth ya kwenye makaratasi ambayo haionekani maishani mwa watu kama serikali ya Mkapa.
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,311
  Trophy Points: 280
  Mkere... umenena kweli lakini wabongo unawajua? Hebu soma hii habari kutoka magazeti ya IPP:

  Sasa wewe jiulize vibudu kama Rostam na Dewji ndio wamepeta hawana akili mzuri...
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hili ni wazo zuri lakini. Siku zote najiuliza kazi ya mbunge hasa ni nini? Sijui jibu nililonalo kama ni jibu sahihi.

  Je Matatizo ya umeme kigoma ni sababu hawakua na wabunge wazuri. Je bara bara za lami na umeme Kilimanjaro vijijini ni KPI kuonyesha wabunge wa moshi ni wamekuwa watendaji wazuri?

  Je kuna wabunge wana ujanja wa kulobby miradi iliyotakiwa kwenda sehemu fulani iende jimboni kwao ? Vipimo vya KPI za wabunge mawaziri zitakuwa sawa na wale wasio mawaziri?Kuna maswali mengi

  Binafsi naona mchango wa wabunge kwenye maendeleo ya wananchi ni mdogo sana. Infact naona bunge la tanzania linatakiw kuwa na wabunge kati ya 100-125.Sababu matatizo tuliyonayo ni yale yale. Ni sehemu chache sana zina area specific problem. Hizi KPI labda tuziweke kwa ma DC na RC

   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Kuna old guard mmoja wa CCM (kati ya Malecela / Kingune/ Rostam nafikiri, can't be sure), aliulizwa anawezaje kuwa mbunge bila kuuliza maswali mengi bungeni? Mbona hasikiki?

  Akajibu na kusema kwamba, kuna backroom dealins na mawaziri zinaweza kuwa muhimu kuliko hata maswali bungeni, na mara nyingi hata wabunge wanaouliza maswali hufanya hivyo kwa show tu, na kwamba mbunge anaweza asisikike bungeni lakini vitu vyake vikaonekana jimboni, na mwingine akasikika sana bungeni, lakini ikawa lip service tu, jimboni hamna kitu.

  Ndiyo mambo ya kina Magufuli hayo, kama waziri huwezi kumsikia anaibana serikali, lakini backroom huko anapiga deals na mawaziri wenzake, hata barabara anaipindisha ipitie jimboni kwake. Sasa utasema mtu kama huyu anahitaji kusikika sana bungeni ?

  Najua it sounds a tad bit unethical kwamba kuna level fulani ya transparency inakosekana, lakini inaonekana ndivyo politics za bongo zinavyoenda.
   
 6. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  mawazo mazuri mdau ila nhi yetu kiziwi kila kitu mpaka kwa hisani ya watu wa marekani
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kama unavyosema ni show wananchi wajisikie kuwa serikali ipo karibu yao lakini hakuna kitu.

  Kwa mahesabu ya haraka nilikuwa naona gharama za mshahara wa mbunge na gharama za uchaguzi za wabunge kwenye jimbo sijui ni shilingi ngapi. But let say kila wilaya inapunguza jimbo Moja. Gharama zinazookolewa zinaweza kujenga visima vya majsafi kwa mwaka katika wilaya. kwa miaka mitano visima 60.

  Je kuna wilaya yeyote tanzania japo inajenga visima 10 vya maji kwa. Je kuna mbunge yuko tayari kusimama bungeni kuomba idadi ya majimbo ipunguzwe ai jimbo lake lifutwe na kuomba pesa zitazookolewa ziingie kwenye miradi ya kuwasaidia wanachi?

  Tanzania sidhani kama tuna area specific problem kiasi kuhitaji kuwa na wabunge wengi kama tulionao. matatizo yetu ni ya msingi, maji,elimu, afya miundombinu, kilimo.

  Wenzetu wanahitaji wabunge wengi sababu matatizo haya walishayamaliza. Kwao kila eneo lina matatizo tofauti. sisi hatujafika uko.

  Napenda nisikie NEC inaachana na hizi siasa za kuongeza majimbo.
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,311
  Trophy Points: 280
  Hawa ni wabunge type ya akina Rostam, Mkono, Dewji na Mramba. Wanaiba bilions wanajenga kashule ka million 10.....
   
 9. M

  Machamle Member

  #9
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kumbuka waswahili husema debe tupu haliachi kutika na simba mwenda kimya ndio mla nyama.Kunyamaza kwa mbunge si kwamba hana kitu.There are a thousand and one ways of doing a thing.
   
Loading...