Wabunge wapewe mafunzo maalum!

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Wafundishwe namna ya kufikiri kabla ya kushangilia au kupiga makofi. Bungeni siyo Kanisa la kiroho ambako mchungaji akinukuu mstari wa Biblia unaokupendeza basi unapiga makofi na vigelegele, tens kwa mzee wa upako unaenda kumtunza kabisa.

Mbunge kabla ya kurukaruka na kugonga Meza ni lazima ajihoji kama jambo hill lina tija kwa mwananchi anayemuwakilisha.

Nimwombe sana katibu wa ubunge ikimpendeza anitafute hata Mimi nitaendesha mafunzo hayo bila malipo yoyote.

Hali niliyoiona Leo kwa baadhi ya wabunge imeonyesha ubinafsi uliopitiliza!
 
Nami nakuuunga mkono mkuu. Sijaona mantiki ya wabunge kushangilia wakati hotuba ya makadirio ya bajeti ikisomwa.
Hasa pale ilipoelezwa na waziri kuwa anapendekeza kufuta road licence. Hapa una waziri anayekuja kuomba kwenu ili apitishe hiyo bajeti tena anatumia neno inapendekezwa ili ninyi mkubali au kukataa lakini wabunge wanashangilia!
Hii inaonyesha kutojiamini au kupigia mstari kile kinachoitwa kuwa rubber stamp ya bunge kwa serikali.
Ni mategemeo yangu kuwa Kwa walichoonyesha bajeti hiyo itapitishwa Kwa asilimia 100, wakati wabunge wanaweza kuikataa au kubadili baadhi ya maeneo na ndio Sababu aliyeisoma amesema hayo ni mapendekezo
Naunga mkono kuwa wabunge wetu wanahitaji kujengewa uelewa juu ya shughuli zao.
Zama za bunge la chama kimoja ilikuwa nafuu kuliko sasa,kwani mawaziri walikuwa wakipata wakati ngumu kupitisha bajeti zao hasa pale wabunge kadhaa walipokuwa wakitoa shilingi. Siku hizi duh
 
Watu wanajiandaa na 2020 wewe unafikiria kufikiria bajeti unacheza na tz wewe.

Mgeni wewe ktk mji huu wa Nazareth?
 
Wafundishwe namna ya kufikiri kabla ya kushangilia au kupiga makofi. Bungeni siyo Manisa la kiroho ambako mchungaji akinukuu mstari wa Biblia unaokupendeza basi unapiga makofi na vigelegele, tens kwa mzee wa upako unaenda kumtunza kabisa. Mbunge kabla ya kurukaruka na kugonga Meza ni lazima ajihoji kama jambo hill lina tija kwa mwananchi anayemuwakilisha.Nimwombe sana katibu wa ubunge ikimpendeza anitafute hata Mimi nitaendesha mafunzo hayo bila malipo yoyote. Haki niliyoiona Leo kwa baadhi ya wabunge imeonyesha ubinafsi uliopitiliza!
Ushangiliaji kama ule huwezi kuuona katika mabunge mengine, mfano kenya na kwingineko. Hawa wa kwetu nadhani kuna kitu hakiko sawa. Baadhi yao tena waliokuwa washangiliaji wakubwa baada ya kumaliza wakatoka nje walihojiwa na wanahabari. Majibu yao aibu tupu!
 
Ulipoona matusi hatukusikia ushauri wako kuwa ukaendeshe mafunzo ya namna ya kufikiri ,leo kugonga meza ndio unaona waheshimiwa wanatakiwa wapate mafunzo sasa ulitaka wagonge masaburi yako kama si kugonga meza?
 
Mwenywe nilisikitika sana yaan Mbunge unasimama kushangilia Budget pendekezwa????

Yaan umepat wap muda kupitia budget yote na kuitafakari kwa kina had ushangalie namna ile????

Kweli maajabu hayataisha Tanzania....
 
Ulipoona matusi hatukusikia ushauri wako kuwa ukaendeshe mafunzo ya namna ya kufikiri ,leo kugonga meza ndio unaona waheshimiwa wanatakiwa wapate mafunzo sasa ulitaka wagonge masaburi yako kama si kugonga meza?
Kwahiyo ukigongwa masaburi huwa unashangilia, hongera zako!
 
Kuna jambo linaniudji sana!!

Akina mama wajawazito wanalala wawili wawili kwenye kitanda ambacho kinamtosha mtu mmoja, wengine wanatandikiwa godoro chini wanalala tena wawili wawili wakiwa kwenye Labour ward(wodi ya akina mama wenye uchungu wa uzazi) kwenye Hospitali ya Taifa, Halafu mijitu inasema haiwezi kutumia prado bali inataka VX au V8 ambayo inagharimu milioni 200? Huu ni wendawazimu uliotukuka. Sijui huwa wanafikiria wao walizaliwa kwenye mazingira gani ambayo yapo bora kushinda sasa ambayo tunajifariji tumepiga hatua japo kuwapatia magodoro walale chini kabla hawajajifungua.

Hao hao ndio leo wanapitisha mambo bila kufikiria faida itakayopatikana kwa wananchi bali wanafanya ili kumfurahisha mtu mmoja tu huku wakisahau waliowapa ridhaa ya kuwawakilisha.

Endeleeni kushangilia na kukubali bila kufikiria, hayo ndio matokeo ya sisi wananchi kutojielewa na kuchagua watu wasiojielewa.
 
Ushangiliaji kama ule huwezi kuuona katika mabunge mengine, mfano kenya na kwingineko. Hawa wa kwetu nadhani kuna kitu hakiko sawa. Baadhi yao tena waliokuwa washangiliaji wakubwa baada ya kumaliza wakatoka nje walihojiwa na wanahabari. Majibu yao aibu tupu!
 
Inaonekana waliandaliwa mapema na kufanya ka "RIHESO" kabisa ka kushangilia.

Wapuuzi sana..!
 
kama hali itaendelea hivi kwa wabunge hawa, itafika mahala wenye hekima na busara hawatagombania nafasi hizi maana mimi naona kama siku hizi wanajidhalilisha hadharani bila hata woga! Ama kweli aibu ni dalili ya busara na kukosa aibu wakati mwingine ni dalili za kuwa mjinga!
 
Back
Top Bottom