Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Kufuatia sakata la kauli ya mbunge wa Ulanga Mashariki Goodluck Mlinga kusema wabunge wa viti maalumu kutoka kambi ya upinzani ili wapate nafasi hiyo lazima waitwe Baby akimaanisha lazima wawe na mahusiano ya kimapenzi na viongozi wao wa juu.
Leo tarehe 12 Mei, 2016 Wabunge 53 wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi wamejitoa rasmi katika Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) wakipinga kauli za udhalilishaji.
===============
Sakata hili lilianzia hapa:
Mbunge wa Ulanga Mashariki, Goodluck Mlinga (CCM), alisema juzi kuwa ili wabunge wa viti maalum kutoka upinzani wapate nafasi hiyo, lazima waitwe baby; akimaanisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na viongozi.
Tafrani hiyo ilianza baada ya kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Viti Maalimu wa Chadema, Sophia Mwakagenda, aliomba muongozo kwa Spika juu ya kauli ya Mbunge huyo wa Ulanga aliyoitoa juzi jioni.
Mwakagenda alisema serikali imeridhia mikataba mbalimbali ikiwamo wabunge kuingia bungeni kwa nafasi mbalimbali, lakini ameshangazwa na kauli ya Kombani kuwa "wanawake wa upande wa Chadema tumeingia (bungeni) kwa sababu ya kuitwa mababy."
Kombani alikuwa akichangia maoni kwenye hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria.
“Rais wetu amefanya vizuri sana katika kutimiza ahadi hii (kuteuwa wabunge), hata wewe amekuteua kuwa mbunge na umesimama kuwa Naibu Spika leo kwa sababu ya mikataba tuliyosaini.
Mwakagenda alitoa maelezo marefu yanayoonyesha uhalali wa kuwapo viti maalumu, ikiwemo kutoa mfano kuwa hata Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson aliyekuwa akiongoza kikao hicho alichaguliwa na Rais John Magufuli kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kabla ya wadhifa wa sasa.
Baada ya maelezo hayo, Naibu Spika alimtaka mbunge huyo aliyeomba muongozo kuketi huku akieleza kuwa suala hilo alishalitoa ufafanuzi juzi.
“Jana (juzi) nilisimama hapa niliposimama sasa hivi baada ya yale maneno na nikasema pande zote mbili zilitumia lugha ambayo siyo nzuri.
“Na nilitoa maelezo kuwa maneno yale yafutwe kwenye taarifa rasmi za Bunge, tukaendelea na tukapitisha bajeti, muongozo wangu ndiyo huo,” alisema Dk. Tulia.
Baada ya kauli hiyo, wabunge wengi wanawake wa upinzani walisimama na kutaka kupewa maelezo zaidi jambo ambalo Dk Tulia aliliktaa.
“Waheshimiwa mliosimama najua mnajua mimi nikisimama mnatakiwa mkae, nilishatolea maelezo jana na leo nimeombwa muongozo nimeshatoa.”
Baada ya maelezo, hayo wabunge wengi zaidi wa upinzani walisimama na kuanza kuomba muongozo huku Dk. Tulia akiwa anasoma matangazo ya siku na kuwatambua wageni waliokuwa bungeni.
Wakati hayo yakiendelea, mbunge mmoja aliwasha kipaza sauti na kumwambia Dk. Tulia kuwa kama wao ni mababy basi yeye ni “ Mkuu wa mababy”.
Baada ya dakika chache, wabunge hao waliketi chini na Dk. Tulia akaendelea kusoma matangazo, huku wale wabunge wa upinzani wakiendele kuzungumza chini chini jambo lililofanya Naibu Spika huyo kusitisha matangazo mara kwa mara na kuwanyamazisha.
Baada ya Dk. Tulia kumaliza kusoma matangazo hayo, wabunge wanawake wa upinzani walinyanyuka tena na kuomba muongozo wa kiti.
Jambo hilo, lilikataliwa tena na Dk. Tulia, hali iliyosababisha waanze kurushiana tena maneno ya kushutumu uamuzi wake .
Wakati Dk. Tulia akiendelea kuwasihi wabunge hao wakae, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, alisikika akimwelieza Naibu Spika aache kutisha wabunge.
Hali ya hewa iliendelea kuchafuka kwa wabunge wengi kusimama na kila mmoja kuwa anazungumza lake, huku Dk. Tulia akiwasii waketi na walipogoma aliwataka kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Dk. Tulia aliwaita askari wa Bunge ili kuwatoa wabunge hao nje ambapo wakati wakitolewa walianza kurusha vitabu na nyaraka nyingine mbalimbali ambazo walikuwa wamepewa.
Wakati wabunge hao wakiendelea kutoka, mbunge mmoja mwanaume ambaye hakufahamika mara moja aliwasha kipaza sauti na kumuliza Naibu Spika "eti wewe ni baby wa nani?"
Mbunge mwingine tena aliwasha kipaza sauti na kusema “mheshimiwa Halima abaki huyo ni mwenzetu”, na mwingine akasema “mheshimiwa Naibu Spika mwambie Halima arudi”.
Baada ya wabunge hao wanawake wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisimama na kuomba mwongozo wa kiti jambo ambalo lilikataliwa.
Kwa sekunde kadhaa Mchungaji Msingwa alibishana na DK. Tulia wote wakiwa wamesimama kabla ya kukubali kuzima kipaza sauti chake.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Mbunge wa Tarime vijijini, (Chadema) John Heche alisimama na kumwambia Naibu Spika kuwa wao wanataka kuzungumza kwa mujibu wa kanuni na kwamba asiwapelekeshe kwa sababu wao siyo wanafunzi wake.
Baada ya kukataliwa kuzungumza wabunge hao wawili pamoja na James Ole Miliya wa Simanjiro, ambaye naye ni wa Chadema, walitoka nje ya ukumbi huo wa Bunge.
Chanzo: IPP Media