Wabunge wanaokataa kukatwa Kodi katika Kiinua mgongo wanapaswa kujiuzulu

May 22, 2016
63
59
WABUNGE WANAOKATAA KUKATWA KODI KATIKA KIINUA MGONGO WANAPASWA KUJIUZURU.

Na Abel Magembe Lugimba.

Nimesikitishwa sana na Baadhi ya wabunge hususani wa chama changu cha CCM kukataa baada ya miaka mitano kwenye kiinua mgongo wasikatwe kodi. Jambo hili sio la kizalendo hata kidogo kabsa, nilishuhudia kwa macho ya nguvu Waziri wa fedha na Mipango alipokuwa anatangaza kufuta misamaha ya kodi katika baadhi ya taasisi za serikali kama vile Jeshi na kwenye taasisi za dini Kwa pamoja walishangilia sana.

Nilitegemea wabunge wa chama changu wangekuwa mstari wa mbele kuiunga mkono serikali yetu katika jambo hili lakini imekuwa vice versa. Baadhi ya Sababu ambazo niwewasikia wakizisema ni kwamba wao wamekuwa kama ATM MACHINE katika majimbo yao, hii inamaana kwamba wao ndio kila kitu kwa wananchi wao inapotokea matatizo kwa wananchi wao huwa wanatoa pesa mifukoni mwao, mimi jambo hili sikubaliani nalo kwani najua namna gani pesa za kiinua mgongo kwa wabunge zimekuwa zikitumika. Ikumbukwe pesa za kiinua mgongo hutolewa baada ya miaka mitano pale Bunge tu linapovunjwa na kila Mbunge hupewa zaidi ya milioni 200 kama kiinua Mgongo, kitu cha kushangaza pesa hizo ndio ambazo zimekuwa zikitumika kuwahonga wapiga kura ili waweze kuwapa ridhaa tena kurudi Bungeni kwa awamu nyingine.

Hii ndio sababu kubwa ambayo hupelekea Kuwepo kwa Rushwa kipindi cha Uchaguzi laiti kama pasingekuwepo na kiinua mgongo kwa wabunge nafikiria hata Rushwa ingeweza kupungua kipindi cha Uchaguzi.Pesa za kiinua mgongo zimewafanya Wabunge baadhi kutowajibika vema kwa wapiga kura wao na kupelekea ikikaribia mwaka wa uchaguzi ndio utawaona wakijifanya kupita kwa wananchi na kuanza kuandaa makundi ya watu huku wakiwapa pesa kwa ajiri ya Kampeni.

Ukifuatilia kwa umakini mkubwa kuhusu wabunge ambao hawataki wakatwe kodi katika viinua migongo utagundua wengi wao ni wale ambao wamezoea kupata Ubunge kwa kutumia pesa nyingi, pia wabunge hawa unapokaribia uchaguzi huchukua mikopo mikubwa kwa mabenki kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huku wakiwa na uhakika kwa wakirudi tena Bungeni wataweza kulipa madeni hayo. Kuna baadhi ya watu walikuwa wamegeuza Bunge kama ni sehemu ya kujinufaisha wao na familia zao..

Wengi wao walikuwa wakishapata Ubunge hawaonekani tena Majimboni mpaka mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ndio unawao wanajisogeza karibu jimboni. Chama cha Mapinduzi tumepoteza majimbo mengi sana kutokana na kuwa na wabunge ambao hawawajibiki ipasavyo kwa wananchi ambo walikuwa wakisubiria ukikaribia uchaguzi ndio wanaonekana majimboni.

Unakuta mbunge mmoja wa CCM katika jimbo fulani hawajibiki kwa wananchi wake kutokana na kusimamia Biashara zake, halafu unakuta viongozi wa CCM katika wilaya ile amewaweka mfukoni mwake kwa sababu yake chama chetu kinachukiwa na wananchi kwelikweli baada ya miaka mitano kwenye kura za maoni anatumia pesa anashinda kwa sababu viongozi wa chama alishawanunua muda mrefu na wanachama,pia hii inapelekea akisimamishwa kama mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika uchaguzi tunashindwa vibaya na Upinzani. Naamini utakapokuwa umepitishwa Bungeni ule mswada unaotenganisha siasa na biashara watu wa aina hii watakuwa wamedhibitiwa ndani ya CCM.

Kama wafanyakazi wengine wa serikali wanakatwa kodi katika viinua migongo yao sasa iweje wabunge wetu wakatae hii inashangaza sana na hapa ndipo utajua ni Wanasiasa wangapi ni Wazalendo.Tafsiri ya wabunge hao kugoma kukatwa kodi huku wakishangilia taasisi zingine kuondolewa kwa misahama ya kodi ni Unafiki. Kubana matumizi, kufuta misamaha ya kodi na kuongeza vyanzo vya mapato haya ni mambo ambayo yapo katika ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020).

Serikali yetu ndiyo inayotekeleza Ilani yetu ya uchaguzi, hiki kitendo cha hawa wabunge ambao mwaka jana walisimama kwa wananchi kuinadi Ilani yetu na kuahidi kuitetea halafu leo baadhi ya mambo yaliyo kwenye ilani wanayakataa hii ni aibu kubwa sana ndani ya CCM.

Serikali hainabudi Kuangalia upya suala la kiinua mgongo kwa wabunge, pamoja na kuamua kufuta msamaha wa kodi bali inatakiwa Ikipunguze kabsa kwani ni kikubwa mno. Mwaka jana wabunge walipata kiinua mgongo kila mmoja TSH 238,000,000/=, kiasi hiki ni kwa miaka mitano tu. Mfanyakazi wa serikali kwa mfano mwalimu anapostaafu kazini serikal hulipwa kiinua mgongo ambacho hakizidi TSH100,000,000/= kama alianza kufanya kazi na miaka 25 inamaana hadi kufika miaka 60 anakuwa ametumika serikali kwa muda wa miaka 35 lakini anaishia kulipwa chini la milion 100.Kwa kawaida mshahara wa Mbunge pamoja na Allowances ni TSH milioni 12 kwa mwezi ambapo kwa muda wa miaka mitano =TSH720,000,000.Jumla ya Kiinua mgongo, mshahara na posho ni Zaidi ya TSH 958,000,000/= kwa kila Mbunge kwa miaka mitano.

Serikali inatakiwa pia kutizama upya suala la posho za vikao vya wabunge (sitting Allowance) TSH220,000/= ..Binafsi sioni umhimu wa wabunge kulipwa pesa hizo kama posho ya makalio,nivema pesa hii ikaelekezwa katika shughuli zingine za kimaendeleo kwa wananchi kwa sababu wanapokea mishahara mikubwa tu kila mwisho wa mwezi. Hivyo Basi ninaomba serikali izifute pesa hizi halafu pia ipunguze kiinua mgongo na kiwe Shilingi milioni 100 au pungufu ya hapo.

Mimi ninafahamu Uongozi sio sehemu ya kujitajirisha bali ni utumishi wa watu, na unapokuwa kiongozi wa Umma hainabudi kutanguliza maslahi ya umma mbele kuliko kuweko maslahi yako mbele kwanza. Ninawaomba wabunge ambao hawataki kukatwa kodi ila wao wanashangilia wanyonge kulipa kodi ni bora wakajiuzuru katika nafasi zao kwani kunawatu wapo tayari kwenda Bungeni kuwawakilisha wananchi bila kutegemea kiinua mgongo wala posho na wakasurvive kwa mishahara tu. Binafsi nipo tayari kuziba pengo hilo kama wataamua kujiuzuru..

Mwisho, Serikali isiwaonee huruma wabunge wanaolalamika kuguswa Maslahi yao, Katika kuleta Usawa na haki kila Mwananchi awajibike kwa nafasi yake katika kulipa kodi kwani hakuna taifa duniani lililoendelea bila kuwabana watu wake kulipa kodi.

Wako,
Abel Magembe Lugimba.
MwanaMapinduzi Mzalendo kutoka mkoa wa Rukwa.
 
Unavyo waona hao wabunge wa ccm jins akili zao zilivyo, hata wew uko hivyo hampishan kabsa, Nao walikuwa kama ww
 
Maghembe nimeupenda uzalendo kwenye andika lako. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema tujisahihishe, ndicho ulichokifanya. Kila mtu anastahili maisha yenye neema, katika kila sekunde anayoishi hapa duniani.

Wala tusidhani kuwa hakuna omba omba huko Marekani/Canada/Ujerumani/Norway/China na kwingineko. Wapo masikini lakini serikali zao hupambana kila inavyowezekana ili keki ya taifa imfikie kila mtu kwa namna moja au nyingine.

Ujanja ujanja upo Afrika na umechangia sana katika kukuza umasikini. Leo hii ndio tunakumbuka madawati!, yote hiyo ni selfishness. Lakini haiwezi kudumu kwa sababu kwenye nchi siku zote ni lazima wataibuka watetezi wa haki kwa maana halisi. Andiko zuri limejikita katika kujenga ule moyo wa kujisahihisha ndani ya CCM yenyewe.
 
Kuna watu wana sifa na nia ya kuwatumikia wananchi hata kwa milioni mbili tu kwa mwezi.
Serikali ikaze kamba.
 
Sasa unazani wakiambiwa wajiuzuru atabaki Nani sasa katika wabunge Wa ccm mwenyekiti Wa bajeti ndio mshika bango ataki wakatwe kodi wabunge wengi Wa ccm wapo kimaslai tu mfano tu hapa jf kuna buku7 FC wamepotea kisa maslai jukwaani awaonekani
 
Yes....wabunge wa Africa hawana huruma kanisa...wanapenda kujipendelea wenyewe tu
 
Hii ndio faida ya kuchagua wabunge wa CCM.Magembe, kwa hawa wabunge wa CCM ni kipi cha ajabu wamefanya mpaka uwashangae kiaisi hiki?Umesahau walidai hata posho ya laki tatu kwa siku katika Bunge la Katiba ilikuwa ndogo?Kabla ya kuendelea kulalamika acheni kwanza kuchagua watu wale wale huku mkitarajia wabadilike.Huu nao ni unafiki kama unafiki mwingine tu.
 
WABUNGE WANAOKATAA KUKATWA KODI KATIKA KIINUA MGONGO WANAPASWA KUJIUZURU.

Na Abel Magembe Lugimba.

Nimesikitishwa sana na Baadhi ya wabunge hususani wa chama changu cha CCM kukataa baada ya miaka mitano kwenye kiinua mgongo wasikatwe kodi. Jambo hili sio la kizalendo hata kidogo kabsa, nilishuhudia kwa macho ya nguvu Waziri wa fedha na Mipango alipokuwa anatangaza kufuta misamaha ya kodi katika baadhi ya taasisi za serikali kama vile Jeshi na kwenye taasisi za dini Kwa pamoja walishangilia sana. Nilitegemea wabunge wa chama changu wangekuwa mstari wa mbele kuiunga mkono serikali yetu katika jambo hili lakini imekuwa vice versa. Baadhi ya Sababu ambazo niwewasikia wakizisema ni kwamba wao wamekuwa kama ATM MACHINE katika majimbo yao, hii inamaana kwamba wao ndio kila kitu kwa wananchi wao inapotokea matatizo kwa wananchi wao huwa wanatoa pesa mifukoni mwao, mimi jambo hili sikubaliani nalo kwani najua namna gani pesa za kiinua mgongo kwa wabunge zimekuwa zikitumika. Ikumbukwe pesa za kiinua mgongo hutolewa baada ya miaka mitano pale Bunge tu linapovunjwa na kila Mbunge hupewa zaidi ya milioni 200 kama kiinua Mgongo, kitu cha kushangaza pesa hizo ndio ambazo zimekuwa zikitumika kuwahonga wapiga kura ili waweze kuwapa ridhaa tena kurudi Bungeni kwa awamu nyingine. Hii ndio sababu kubwa ambayo hupelekea Kuwepo kwa Rushwa kipindi cha Uchaguzi laiti kama pasingekuwepo na kiinua mgongo kwa wabunge nafikiria hata Rushwa ingeweza kupungua kipindi cha Uchaguzi.Pesa za kiinua mgongo zimewafanya Wabunge baadhi kutowajibika vema kwa wapiga kura wao na kupelekea ikikaribia mwaka wa uchaguzi ndio utawaona wakijifanya kupita kwa wananchi na kuanza kuandaa makundi ya watu huku wakiwapa pesa kwa ajiri ya Kampeni.

Ukifuatilia kwa umakini mkubwa kuhusu wabunge ambao hawataki wakatwe kodi katika viinua migongo utagundua wengi wao ni wale ambao wamezoea kupata Ubunge kwa kutumia pesa nyingi, pia wabunge hawa unapokaribia uchaguzi huchukua mikopo mikubwa kwa mabenki kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huku wakiwa na uhakika kwa wakirudi tena Bungeni wataweza kulipa madeni hayo. Kuna baadhi ya watu walikuwa wamegeuza Bunge kama ni sehemu ya kujinufaisha wao na familia zao.. Wengi wao walikuwa wakishapata Ubunge hawaonekani tena Majimboni mpaka mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ndio unawao wanajisogeza karibu jimboni. Chama cha Mapinduzi tumepoteza majimbo mengi sana kutokana na kuwa na wabunge ambao hawawajibiki ipasavyo kwa wananchi ambo walikuwa wakisubiria ukikaribia uchaguzi ndio wanaonekana majimboni. Unakuta mbunge mmoja wa CCM katika jimbo fulani hawajibiki kwa wananchi wake kutokana na kusimamia Biashara zake, halafu unakuta viongozi wa CCM katika wilaya ile amewaweka mfukoni mwake kwa sababu yake chama chetu kinachukiwa na wananchi kwelikweli baada ya miaka mitano kwenye kura za maoni anatumia pesa anashinda kwa sababu viongozi wa chama alishawanunua muda mrefu na wanachama,pia hii inapelekea akisimamishwa kama mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika uchaguzi tunashindwa vibaya na Upinzani. Naamini utakapokuwa umepitishwa Bungeni ule mswada unaotenganisha siasa na biashara watu wa aina hii watakuwa wamedhibitiwa ndani ya CCM.

Kama wafanyakazi wengine wa serikali wanakatwa kodi katika viinua migongo yao sasa iweje wabunge wetu wakatae hii inashangaza sana na hapa ndipo utajua ni Wanasiasa wangapi ni Wazalendo.Tafsiri ya wabunge hao kugoma kukatwa kodi huku wakishangilia taasisi zingine kuondolewa kwa misahama ya kodi ni Unafiki. Kubana matumizi, kufuta misamaha ya kodi na kuongeza vyanzo vya mapato haya ni mambo ambayo yapo katika ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020).Serikali yetu ndiyo inayotekeleza Ilani yetu ya uchaguzi, hiki kitendo cha hawa wabunge ambao mwaka jana walisimama kwa wananchi kuinadi Ilani yetu na kuahidi kuitetea halafu leo baadhi ya mambo yaliyo kwenye ilani wanayakataa hii ni aibu kubwa sana ndani ya CCM.

Serikali hainabudi Kuangalia upya suala la kiinua mgongo kwa wabunge, pamoja na kuamua kufuta msamaha wa kodi bali inatakiwa Ikipunguze kabsa kwani ni kikubwa mno. Mwaka jana wabunge walipata kiinua mgongo kila mmoja TSH 238,000,000/=, kiasi hiki ni kwa miaka mitano tu. Mfanyakazi wa serikali kwa mfano mwalimu anapostaafu kazini serikal hulipwa kiinua mgongo ambacho hakizidi TSH100,000,000/= kama alianza kufanya kazi na miaka 25 inamaana hadi kufika miaka 60 anakuwa ametumika serikali kwa muda wa miaka 35 lakini anaishia kulipwa chini la milion 100.Kwa kawaida mshahara wa Mbunge pamoja na Allowances ni TSH milioni 12 kwa mwezi ambapo kwa muda wa miaka mitano =TSH720,000,000.Jumla ya Kiinua mgongo, mshahara na posho ni Zaidi ya TSH 958,000,000/= kwa kila Mbunge kwa miaka mitano.

Serikali inatakiwa pia kutizama upya suala la posho za vikao vya wabunge (sitting Allowance) TSH220,000/= ..Binafsi sioni umhimu wa wabunge kulipwa pesa hizo kama posho ya makalio,nivema pesa hii ikaelekezwa katika shughuli zingine za kimaendeleo kwa wananchi kwa sababu wanapokea mishahara mikubwa tu kila mwisho wa mwezi. Hivyo Basi ninaomba serikali izifute pesa hizi halafu pia ipunguze kiinua mgongo na kiwe Shilingi milioni 100 au pungufu ya hapo.

Mimi ninafahamu Uongozi sio sehemu ya kujitajirisha bali ni utumishi wa watu, na unapokuwa kiongozi wa Umma hainabudi kutanguliza maslahi ya umma mbele kuliko kuweko maslahi yako mbele kwanza. Ninawaomba wabunge ambao hawataki kukatwa kodi ila wao wanashangilia wanyonge kulipa kodi ni bora wakajiuzuru katika nafasi zao kwani kunawatu wapo tayari kwenda Bungeni kuwawakilisha wananchi bila kutegemea kiinua mgongo wala posho na wakasurvive kwa mishahara tu. Binafsi nipo tayari kuziba pengo hilo kama wataamua kujiuzuru..

Mwisho, Serikali isiwaonee huruma wabunge wanaolalamika kuguswa Maslahi yao, Katika kuleta Usawa na haki kila Mwananchi awajibike kwa nafasi yake katika kulipa kodi kwani hakuna taifa duniani lililoendelea bila kuwabana watu wake kulipa kodi.

Wako,
Abel Magembe Lugimba.
MwanaMapinduzi Mzalendo kutoka mkoa wa Rukwa.

tena wasirudi tena bungeni
 
Hebu mtu ambaye anafahamu hii ishu ya kiinua mgongo anisaidie kidogo nielewe.

1.Je ni hiki kiinua mgongo kinatokana na hela inayokatwa kwenye mshahara wa mbunge kila mwezi na kukusanywa kwa miaka mitano?

2. Kama kinakatwa kwenye mshahara, kinakatwa kabla au baada ya PAYE kukatwa?

3. Au ni kwamba kiinua mgogo hakitoki kwenye mshahara..badala yake kila baada ya miaka mitano serikali inatafuta 238M ya kumlipa kila mbunge?

Nauliza hivyo kwasababu kama kiinua mgongo kinatokana na makato kwenye mshahara wa kila mwezi..tena kinakatwa baada ya kulipa PAYE...basi kukitoza kodi kiinua mgongo itakua sio haki kwasababu kitakua kimeshalipiwa kodi (double taxation). Ila kama kinatokana na makato ya mshahara KABLA ya kukatwa PAYE au kama ni hela ambayo haitoki kwenye makato ya mshahara..hapo kwakweli inabidi kodi ikatwe, msamaha usiwepo.
 
KILA PATO LAKE LAZIMA LIKATWE KODI,NA PATO LA BAADA YA MIAKA MITANO PIA LAPASWA KUKATWA,
 
KILA PATO LAKE LAZIMA LIKATWE KODI,NA PATO LA BAADA YA MIAKA MITANO PIA LAPASWA KUKATWA,

Mkuu tuambiane ukweli, kama serikali inakata kiasi kwenye mshahara wa mbunge baada ya kumtoza PAYE...na kukusanya hicho kiasi ambacho kimehalipiwa kodi kila mwezi kwa miaka mitano na kisha kumrejeshea mbunge kama kiinua mgongo...itakua si haki kumtoza kodi tena hela ambayo ilishalipiwa kodi awali...yaani utakua unamtoza kodi hiyo hiyo mara mbili. Na hii sio kwa mbunge tu...ni kwa mfanyakazi yoyote yule. Ndio maana nikataka mtu anieleweshe vizuri. Sitetei wabunge kutolipa kodi..ninachopinga ni kulipa kodi hiyo hiyo mara mbili (double taxation).
 
Ukiiangalia bajeti hii kwa undani utakuta ina mambo mengi ambayo yanahitaji kufumuliwa na kurekebishwa lakini Serikali imechomekea kipengele cha mafao ya wabunge makusudi ili waachane na yale muhimu na kupambana na mafao yao,

na kweli bunge hili la chama kimoja wazee wa ndio hakuna lolote wanalojua zaidi ya mafao yao tu.

Yani hata siku 300 bado hawajatimiza wanaongelea eti mafao. Yani wananchi tujiandae kipindi kigumu kama ile miaka 7 ya njaa misri.
 
Kiinua mgongo kisiwepo mpaka mtu afikishe 60years regardless ya kuwa ni mwanasiasa, mwajiriwa au yupo kibinafsi....ni abuse y concept kumpa mtu kiinua mgongo kila baada ya miaka 5...na isiishie hapo tu pia kama wanapata income lazima walipe kodi kwani kila kipato lazima kilipiwe kodi....kwani wao hawapati public service? Hatatuwezi kuendelea iwapo hatutawajibika kama taifa.
 
Back
Top Bottom