Wabunge wamkataa Naibu Waziri

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Wabunge wamkataa Naibu Waziri
Send to a friend
Monday, 24 October 2011 20:39
0digg

12mkulobajetii.jpg
Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo alipokuwa akiingia kwenye viwanja vya BUnge mjini Dodoma tayari kusoma bajeti ya Serikali mwaka 2010/2011

WAMWEKA MKULO KITIMOTO KUHUSU MFUMUKO WA BEI, HALI NGUMU YA MAISHA
Ramadhan Semtawa
WABUNGE wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana, waligoma kuzungumza na Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima na kushinikiza waziri wa wizara hiyo Mustafa Mkulo, kufika mbele ya kamati hiyo kujibu hoja mbalimbali za msingi ikiwemo kuyumba uchumi wa nchi kunakosababishwa na tatizo la mfumuko bei.Tukio hilo limekuja siku ya kwanza ya vikao vya Kamati za Bunge, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya Mkutano wa Tano wa Bunge la Kumi, utakaoanza Novemba 8 mwaka huu mjini Dodoma.

Mfumuko wa bei umetikisa karibu nchi zote Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki( EAC) ukiacha Rwanda yenye ahueni kidogo, na kusababisha kupanda kwa hali ya maisha, huku bei za bidhaa mbalimbali madukani vikiwemo vyakula, zikipaa siku hadi siku.

Takwimu zinaonyesha mfumuko wa bei kwa Tanzania umefikia asilimia 16.8 , huku Uganda ukigota asilimia 28.3 , Kenya asilimia 17.3, Burundi asilimia 11.7 na Rwanda asilimia 6.6

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kamati hizo, jana asubuhi Kamati ya Fedha na Uchumi ilikuwa ilikutane na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mkulo pamoja na watendaji kadhaa wa idara zilizo chini ya wizara hiyo.


Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida, muda wa kuanza kikao ulipofika, hakikuendelea kutokana na kile kilichoelezwa, wajumbe wa kamati kugoma wakitaka Waziri Mkulo mwenyewe awepo ili ajibu hoja nzito zinazohusu uchumi wa nchi . Hadi kufikia saa 4.00 kikao hicho kilikuwa hakijaanza.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk Abdallah Kigoda alipoulizwa, alikiri kumtaka Mkulo mwenyewe awepo kwenye kikao hicho na si naibu wake, Silima. "Ndiyo, tunamtaka (Mkulo) na tunamsubiri yeye kwani si ndiye waziri au ulitakaje?" Alihoji Dk Kigoda ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Uchumi na Mipango kwenye Serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa.

Dk Kigoda ambaye pia ni Mbunge wa Handeni (CCM) alifafanua kwamba, baada ya wao kumtaka waziri afike akiwa na ujumbe wake, walielezwa angekuja jioni mbele ya Kamati baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokuwa kinafanyika Ikulu.

"Tumeambiwa waziri atakuja mwenyewe jioni. Kwa hiyo tunachofanya sasa ni kumsubiri hadi atakapokuja. Sasa kuuliza kwanini hatukuongea na naibu utakuwa unanibana tu kwasababu sisi tunamsubiri waziri mwenyewe,"alisisitiza Dk Kigoda.

Awali, Naibu Waziri Silima aliongoza ujumbe kutoka wizara hiyo na idara zake wakiwemo watendaji wa ngazi za juu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na Kamishna Mkuu, Harry Kitilya na maofisa wengine waandamizi wa Hazina.

Hata hivyo, kabla ya kuruhusiwa kuingia na ujumbe huo wajumbe wa kamati waliomba kuongea na Naibu Waziri huyo huku ujumbe wake ukibaki, mapokezi kuu ya Ofisi ndogo za Bunge.

Wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge, wajumbe walimtaka Naibu Waziri huyo awasiliane na Waziri wake kwani ndiye waliyekuwa wakimhitaji zaidi katika mkutano huo. Wakati hayo yakiendelea ujumbe wa Silima uliendelea kubaki mapokezi kusikilizia kinachoendelea.

Saa 5:30, Silima alitoka nje ya ukumbi huo katika kile kilichodhihirisha ni kufanya mawasiliano na Mkulo ambaye alikuwa Ikulu. Baada ya muda mfupi alirejea na kukaa na Mwenyekiti, Dk Kigoda.

Dakika chache baadaye ujumbe huo wa wizara ukiongozwa Silima na watendaji hao wa idara, uliingia ndani ya ukumbi na kupewa taarifa kwamba kikao hicho kimeahirishwa hadi Waziri Mkulo atakapofika.

Baada ya taarifa hiyo, ujumbe huo wa wizara uliondoka ukumbini, kila mmoja akiwa amebeba mkoba wake tayari kurejea eneo lake la kazi kusubiri maelekezo zaidi ya kikao hicho.


Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, alisema uamuzi wao ulizingatia mambo ya msingi ambayo ni hali halisi ya uchumi wa nchi kwa sasa ambao unatikiswa na kasi kubwa ya mfumuko wa bei.

Mjumbe huyo alifafanua kwamba, katika mazingira magumu kama haya, ni vigumu kukutana na Naibu Waziri pekee ambaye mambo mengi atakayoelezwa, atayaweka kiporo ili ayawasilishe kwa waziri wake.

"Tumemwambia aje na waziri wake kwasababu kuna mambo ambayo tunataka tumweleze waziri mwenyewe na atujibu hapo hapo. Huyu ni naibu tunaweza kumwambia hili akasema atalifikisha kwa waziri, sasa hiyo hatutaki," alifafanua mjumbe huyo.

Alisema mfumuko wa bei uliopo nchini na unaozunguka karibu ukanda wote wa EAC, ni jambo linahotaji maelezo ya kina kutoka kwa waziri mwenyewe na kusisitiza kwamba; "Siyo tunasema halafu tuambiwe taarifa atafikishiwa waziri".

Vikao vya kamati za Bunge vimeanza ambavyo pamoja na mambo mengine, vitajadili mambo mbambali ya kisekta kabla ya kuanza kwa Mkutano wa tano wa Bunge la 10 unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Hata hivyo wakati tukienda mitamboni jana jioni majira ya saa 10: 25, Waziri Mkulo alifanikiwa kufika ukumbi huo ofisi ndogo za Bunge kutana na Kamati hiyo katika kikao kilichoendelea hadi usiku.
 
Back
Top Bottom