Ni ushauri mzuri, ila tatizo nionalo mimi ni kwamba watakaokuwa wanapata mishahara mikubwa sana (kwa professional zao) wanaweza kutumia nguvu kwa pesa kuwa na influence katika eneo hili la maamuzi. Nionalo mimi ni mishara ya wabunge iwe fixed (sawa kwa wote) ila mwenye taaluma ya kitu zaidi (mfano injinia, mkemia, mchumi n.k) kama anatenda professional yake kupitia sekta au kamati ya bunge apewe mshahara zaidi kulingana na matumizi ya hiyo profession na qualification yake. Kama hana anachochangia basi apate tu huo mshahara wa ubunge. Kwa njia hiyo wabunge hawataua career zao kama ilivyo sasa ambapo magwiji wa professions wanajimaliza kitaaluma kupitia siasa za kitumwa tulizorithi kutoka kwa waliotutawala.