tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,852
Wabunge wamelalamikia adhabu aliyopewa kijana wa Arusha aliyemtukana rais kuwa ni ndogo kwa kuwa mhalifu alipewa alipe kiasi cha fedha na kulipa kwa mafungu kwa kuwa alitenda kosa kubwa la kumdhalilisha mtu wa juu katika nchi hii
==========
My Take
Wabunge kuhoji Mamlaka ya Mahakama ni dalili mbaya ya Udikteta. Mahakama inapotoa Hukumu halafu anaibuka Mbunge wa CCM anahoji hukumu hiyo, kisha Waziri wa Sheria anaahidi kuileta hukumu Bungeni ni dalili mbaya sana kwa Utawala wa Sheria.
Hayo yemetokea leo Bungeni Dodoma, wakati Mbunge wa CCM Livingstone Lusinde alipohoji uhalali wa hukumu halali ya Mahakama dhidi ya Kijana aliyeshtakiwa kwa kumkashifu JPM. Kama serikali haijaridhika na hukumu basi ifuate sheria kwa kukata rufaa.
June 21, 2016 Mbunge wa Nchemba, Juma Nkamia alisimama bungeni kuomba mwongozo wa bunge kujadili tukio la mtuhumiwa wa kesi ya kumtukana Rais Magufuli kuchangiwa fedha na watu kwa ajili kulipa fidia, kitendo kinachoashiria dharau. Mwongozo wa Nkamia ukaungwa mkono pia na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde.
Nkamia alisema. "Kuna mtu alimtukana Rais na akahukumiwa kwenda jela au kulipa faini ya milioni 7, alilipa nusu ya faini ile na akaruhusiwa aondoke akatafute fedha nyingine. Nilitaka wanasheri watusaidie, hivi kumtukana Rais wa nchi alafu yule aliyetukana anaruhusiwa akatafute fedha za kulipa" –Juma Nkamia
‘Siku ya kukabidhiwa fedha anaita na waandishi wa habari, na baadhi ya wabunge humu ndani wa chama fulani walionyesha wananchangia fedha yule mtu ili akalipe faini. Kwahiyo ni maana kuwa alitumwa na chama hicho akamtukane Rais.’ –Juma Nkamia
‘Sasa naomba kujua sio dharau kwa Rais? sheria inaruhusu jambo hili kufanyika? na kama mimi leo nikahukumiwa kwa kesi ya kuiba kuku siwezi kuruhusiwa kutafuta fedha, iweje mtu huyu akaruhusiwa kutoka nje kutafuta fedha na bado akaonekana watu wakimkabidhi fedha? hizi ni dharau kwa taifa kwa ujumla‘ –Juma Nkamia
Sasa wataalam naomba mtueleze bunge lina legitimacy ya kujadili mchakato wa utekelezwaji wa hukumu iliyotolewa na muhimili tofauti usioingiliana kikatiba?
Alafu kwanini anataka kujadili hii hukumu wakati huu ambapo watu wameonekana kumchangia kiasi Fulani kilichobakia na wala sio Mara baada ya hukumu kutolewa?