Wabunge waivamia Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge waivamia Simba

Discussion in 'Sports' started by nngu007, Oct 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Zahoro Mlanzi

  WABUNGE wanne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wameibukia katika Kamati mbalimbali mpya za Klabu ya Simba, zilizoundwa
  kushughulikia masuala ya uwekezaji na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa timu hiyo.

  Wabunge hao ni Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Amos Makalla Mbunge wa Mvomero, Richard Ndassa Mbunge wa Sumve na Muktadha Mangungu Mbunge wa Kilwa Kaskazini.

  Mbali na hilo, klabu hiyo pia imepanga kuvunja jengo lao la sasa lililopo makao makuu Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam na kujenga ghorofa la ghorofa 12.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage alisema mwezi mmoja uliopita walivunja Kamati ndogondogo, ili wapate nafasi ya kufanya kazi vizuri zaidi lakini hivi sasa wameamua kuja na kamati nyingine ambazo ni maalumu.

  "Katika kikao chetu cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Oktoba 15, mwaka huu tulikubaliana kuwa na Kamati Maalumu za Ufundi, Mashindano, Fedha, Usajili na Nidhamu zikiwa katika sura na mitizano tofauti," alisema Rage.

  Alisema kwa upande wa Kamati ya Fedha itakayoongozwa na Mwenyekiti, Geofrey Nyange 'Kaburu' akisaidiwa na Adam Mgoyi na wajumbe ni Mbunge Zitto, Juma Pinto, Said Pamba, Abdul Mtengeta na Mbunge Mangungu na Kamati ya Nidhamu itaongozwa na Peter Swai, Jamal Rwambow, Charles Keyela, Chaurembo na Evody Mmanda.

  Alisema Kamati ya Mashindano itakuwa chini ya Joseph Itangile akisaidiwa na Azim Dewji, Jerry Ambi, Swedi Nkwabi, Mbunge Ndassa, Hassan Othman 'Hassanoo', Mohamed Nassor na Mbunge Makalla.

  Kwa upande wa Kamati ya Ufundi, Rage alisema itaongozwa na Ibrahim Masoud 'Maestro', Danny Manembe, Khalid Abeid, Musley Ruwehi, Said Tuli, Mulamu Nga'mbi, Rodney Chiduo na Patrick Rweyemamu.

  Kamati ya Usajili itakuwa na Zakaria Hanspope (Mwenyekiti), Kassim Dewji, Francis Waya, Salim Abdallah, Gerald Lukumay, Collins Frisch na Crensencius Magori.

  Alisema tayari viongozi hao wameshapatiwa taarifa na kwamba jana jioni alitarajia kukutana nao ili kubadilishana mawazo na kupeana majukumu.

  Katika hatua nyingie, Rage alisema wameshaanza kufanya mazungumzo na benki mbili juu ya kuziomba msaada, ili kusaidia kujenga ghorofa refu zaidi.

  Alisema jengo lao la hivi sasa halina hadhi ya timu hiyo na kwamba, wana mpango wa kutengeneza jengo la ghorofa 12 kwenda juu.
   
 2. a

  ablood8 Senior Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Huyo Rage kuahidi tuuu kila siku ahadi Mara uwanja wa kisasa Bunju,mara jengo la ghorofa 12,wakati hili lililopo hata rangi ameshindwa kulipaka.
  Tunataka Vitendo na sio kupiga MUDOMO.
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  title yako sijaielewa................kwani wabunge gawapaswi kua wanachama au washabiki wa timu fulani???
   
Loading...