Wabunge wahuzunika baada ya sekta ya Afya kuongoza kwa wingi wa vyeti feki

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
279
c7d1bed2cf5d3e9455d4cb159589fd6f.jpg

Wabunge wahuzunika baada ya sekta ya Afya kuongoza kwa wingi wa vyeti feki.

Hayo yameelezwa ikiwa ni siku chache baada ya waziri KAIRUKI na serikali kwa ujumla kutoa majina ya jumla ya watumishi 9932 ambapo wengi wa wenye vyeti feki wanatoka sekta ya Afya

Sekta ya Afya ndo nguzo kubwa hasa kwa taifa kwa ujumla kwa maendeleo ya Taifa na vijana wake.

Nini maoni yako katika hili? Serikali ifanyaje kuiboresha sekta hii nyeti?
 
Afya wanajidai wao ni majembe
Kumbe tumejua afya ni uchochoro wa ubar@she.te
Haiwezekani mamishahara makubwa kumbe vyeo sifuri kabisa.
Hizi sekta za umma mshahara ungetakiwa uwe sawa katika level moja ya elimu
Umeanza vzr ukamalizia kwa kuharisha
 
Swali ni watumishi wa afya kiasi gani wana vyeti feki kati ya idadi ya jumla ya watumishi wa afya?
 
Unajuaje kwamba hiki cheti ni feki na hiki si feki ilakuna mchanganyiko mwingine tu 9mtu kabadili jina baada ya kuolewa na hakuripoti inavyotakiwa, mtu kajipindua rekodi zimepotea tu etc)
 
Mtoa mada nataka nikufahamishe kuhusu idara ya afya ili ujue:-
1. Afya kuna
a. Clinicians (A. clinical officer, Clinical officer, Assistant medical officer, MD na Specialists)
b. Laboratory Technologist (Assistant Lab. Tech, Laboratory Tech, Lab. Scientist)
c. Pharmacy Technologist (Assistant Pharm Tech, Pharm Tech na Pharmacist)
d. Nursing (Enrolled Nurse, Registered Nurse na Nursing Officer)
e. Physiotherapist - Kama nilivyoainisha kwa kada zingine
f. Dental - Kama nilivyoainisha
G. Katibu wa Afya
H. Medical attendants

Sasa kwa ufafanuzi huo, ilitakiwa usema ni kundi lipi kati ya hayo. Tambua kuwa hizo ni course tofauti na zinamiongozo tofauti na kila kundi lina usajili wake.

Sasa tueleze ni aina ipi iliyoathirika zaidi kwenye mchakato wa Fyeti feki.

Yaani taaluma kama Clinicians, Laboratory na Dental huwezi kupindisha, ni lazima ufuate track.
 
Sana hapo naona hawa wauguzi wengi watakuwa na vyeti feki. Credit za kuingia uuguzi ni mtu awe na D za PCB. Hiki ni kigezo cha chini sana kwa mtu atakaye shughulikia afya za watanzania. Tena hawa wanakula pesa ya kutosha kama walifaulu vile.
 
Wauguzi wanasoma mpaka distant learning, kama wanavyosoma course zingine ambazo sio za science
 
Mtoa mada nataka nikufahamishe kuhusu idara ya afya ili ujue:-
1. Afya kuna
a. Clinicians (A. clinical officer, Clinical officer, Assistant medical officer, MD na Specialists)
b. Laboratory Technologist (Assistant Lab. Tech, Laboratory Tech, Lab. Scientist)
c. Pharmacy Technologist (Assistant Pharm Tech, Pharm Tech na Pharmacist)
d. Nursing (Enrolled Nurse, Registered Nurse na Nursing Officer)
e. Physiotherapist - Kama nilivyoainisha kwa kada zingine
f. Dental - Kama nilivyoainisha
G. Katibu wa Afya
H. Medical attendants

Sasa kwa ufafanuzi huo, ilitakiwa usema ni kundi lipi kati ya hayo. Tambua kuwa hizo ni course tofauti na zinamiongozo tofauti na kila kundi lina usajili wake.

Sasa tueleze ni aina ipi iliyoathirika zaidi kwenye mchakato wa Fyeti feki.

Yaani taaluma kama Clinicians, Laboratory na Dental huwezi kupindisha, ni lazima ufuate track.
Well narrative!!
Waache biashara ya generalization!!!....huwezi kua daktari kwa vyeti vya kufoji...semester ya kwanza lazima ikutoe knockout
 
Kati ya hao wa afya wengi ni medical attendants (WAHUDUMU WA AFYA- uniform ya kijani iliyofifia). Masomo yao ni ya mwaka mmoja baada ya form four. Kazi yao kuu ni usafi na kuelekeza wagonjwa maeneo mbalimbali ya hospital kama hawapajui. Lakini kutokana na uhaba wa watumishi wa afya, maeneo mengine wamekuwa wakifanya shughuli amabazo sio majukumu yao.
KUwa wengi ni kutokana na serikali kuruhusu au kutozuia au kutokagua vyuo kibao ambavyo vilijinadi kutoa kozi hizo hapo miaka ya nyuma.Vyuo hivi vilikuwa vinadahili wengi wasio kuwa na sifa, hivyo kupokea hata wenye vyeti feki pia au kumfanya ambaye ashasoma hapo ashawishike kutafuta cheti feki kwani hatopata ajira baada ya masomo yake. Wazazi wameliwa sana ada na vyuo hivi. Lakini pia serikali inapenda sana kuajiri kada hii kwani wengi salary ndogo hivyo kubeba mzigo mdogo katika kuwalipa. Halimashauri zikiomba watumishi 50,kati yao hamna ombi la Medical attendants, hupelekewa watumishi 11 (8 medical attendants), Then madiwani +wananchi hupiga makofi na kuipongeza serikali kwa kuletewa watumishi wa afya.
Kwa nurses, waliopatikana na kimbuga hiki, wengi wao ni watu wazima 50+,walisoma uuguzi na ukunga kwa miaka minne baada ya kumaliza darasa la saba.Walisoma na kupata ajira kabla ya takwa la FORM FOUR ktk utumishi wa umma. Walipohitaji kujiendeleza au takwa la cheti hiki lilipowekwa wakaona isiwe taabu wakaingia msituni/mtaani wakaibuka na cheti cha nguvu cha form form. Lakini ni wachapa kazi na wajuzi kuliko hawa dot com wa miaka miwili baada ya form 4(diploma).
COs, AMO na MDs (hasa walioupgrade kutoka CO/AMO to MD) nimewaona ona.
 
Back
Top Bottom