Wabunge Wafanyabiashara wa Mafuta "waihujumu" EWURA

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
Baada ya tuhuma ya rushwa kwa wabunge kusambaa,sasa wabunge wafanyabiashara wa mafuta wametajwa kusuka zengwe ili kuiua EWURA na hivyo kurudisha tabia yao ya uchakachuaji wa mafuta.Uchunguzi uliofanywa na gazeti la JAMHURI unaonyesha kuwa wabunge wenye maslahi katika biashara ya mafuta walianzisha zengwe kwenye kamati ya Nishati na Madini ili kuivunja EWURA.Hoja walizojenga ni kuwa EWURA badala ya kuweka vinasaba kwenye mafuta ya ndani basi waweke kwenye mafuta yanayouzwa soko la nje na hoja nyingine ni kuwa EWURA Wanafanya kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na TRA.

Wabunge wanaosadikiwa kuanzisha zengwe hili ni Catherine Magige ambaye aliombwa na Ahmed Shabby (Shabiby) ambaye alitaka EWURA ifutwe au iondoe vinasaba vya mafuta ya soko la ndani,Magige alipoulizwa alikiri kuwa aliagizwa na Shabiby,lkn akasema si yeye tu bali wabunge wengi wa kamati hiyo walipewa ujumbe na Shabiby jinsi ya kuishughulikia EWURA.Kati ya Wabunge 16 wa kamati hiyo wabunge 14 walisema kazi zinazofanywa na EWURA kwa sasa zinastahili kufanywa na TRA.Wabunge Haroon Mulla Pirmohamed(CCM),Vedasto Mathayo Manyinyi(CCM) na Ally Kessy(CCM) walieleza nia yao ya kupinga vinasaba ktk mafuta yanayouzwa ndani ya nchi.

Uchunguzi wa JAMHURI umegundua kwanza Mathayo Manyinyi ni muuzaji wa mafuta,lkn si hilo tu bali kituo chake cha mafuta kilichopo Musoma ni kati ya vituo vilivyokutwa vinauza mafuta yasiyo na vinasaba na kikapigwa faini ya shilingi milioni 7.Sheria ya EWURA inasema muuza mafuta akiuza bila kuwa na vinasaba anatozwa faini ya kati ya milion 5 hadi 7,kikirudia mara ya pili inakuwa milioni 25 na mara ya tatu kikiuza mafuta bila vinasaba kinafungiwa.Kati ya vituo vilivyotajwa kuuza mafuta yanayopaswa kusafirishwa nje ya nchi ni pamoja na kituo cha Mbunge wa Gairo Ahmed Shabby na cha Manyinyi.Hii iliwafanya wabunge hawa kuanza vita ya kuifuta EWURA,Mbunge wa Gairo kituo chake kimeshakutwa mara ya tatu na kulipa milion 25 hivyo hatua inayofuatia ni kukifungia.

Shabiby alipoulizwa akasema anapinga uwepo wa UWURA sababu wanahujumu biashara za wafanyabiashara wadogo wa mafuta kama yeye,na anasema swala hilo amelipeleka kwa Waziri Mkuu Majaliwa na Wziri wa Nishati Muhongo ili asaidiwe.Shabiby anasema vinasaba vimekuwa vinauzwa mtaani kwa ghalama ya shilingi milioni 2 kwa lita, na wateja wa hivyo vinasaba ni wafanyabiashara wakubwa wa mafuta wanaonunua na kuweka ktk maghala yao na hivyo kutumia kwa yale mafuta yasiyolipiwa ushuru yanayopaswa kusafirishwa nje ya nchi.

Ripoti ya Utafiti iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Dsm inaonyesha kuwa tangu mwaka 2011 Ewura ilipoanza kuweka vinasaba kwenye mafuta,kiwango cha kodi kimeongezeka kwa shilingi bilioni 468.50,na pia imesaidia mteja kupata mafuta yenye ubora na takwimu halisi ya kiwango cha matumizi ya mafuta nchini.
Hivyo hoja ya Wabunge hao isiyo ya kitafiti inamezwa na hoja ya kitafiti ya chuo kikuu cha Dsm.Hali hii ya Wabunge wenye maslahi ktk sekta ya mafuta kuwa wajumbe wa kamati zinazohusu Nishati hii ni mgongano wa kimaslahi na mwanya wa uhujumu wa uchumi.Bunge litazame upya namna ya kuwapanga wabunge ktk kamati na kuondoa mgongano wa maslahi.
 
Hao wabunge majina yao yakiwekwa hadharani utakuta wote ni ccm believe me I tell you
Upigaji hauna chama wala dini wala kabila. Nyie ndio mnaanza ujinga wa kugawa watu kwa misingi ya vyama na mwisho wake mafisadi ndio wanashinda. Hta upinzani wapo wapiga dili wengi. Inatakiwa wote tujipange bila kuangalia chama cha mkosaji.
 
ila kwa kweli tumepumzika sana kuuziwa mafuta yaliyochakachuliwa, hata zile yard zilizokuwa pembezoni ya Kibaha - Chalinze naona zimepata natural death. Sasa huyu Shabiby mbona sisi huku Gairo hatukumtuma akatuwakilishe hivyo... anataka kuturudisha wapi tena?
 
Shabiby anatafuta cha kutafuta, subiri atengeneze bomu limlipue mwenyewe! Wampe kesi moja tamu sana ya kuhujumu uchumi wa nchi hapo atatulia! Anataka ku destabilize state organs and machinery kwa manufaa binafsi! Asubiri tu kama hamjui vizuri JPM aliejeruhiwa na kukatwa misaada asubiri!
 
Back
Top Bottom