Wabunge wa Z’bar warushiwa Kombora na Wawakilishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa Z’bar warushiwa Kombora na Wawakilishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 23, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][​IMG][/h]
  Na Mwinyi Sadallah

  23rd June 2012
  Sakata la kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, limechukua sura mpya baada ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW), kulalamika kuwa wabunge kutoka Zanzibar wamekuwa mzigo kutokana na kushindwa kutetea maslahi ya Zanzibar katika mfumo wa muungano huo.
  Tamko hilo wamelitoa walipokuwa wakichagia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2012/2013 katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi, kinachoendelea Chukwani mjini Zanzibar jana.
  Akichagia bajeti hiyo Mwakilishi wa Jimbo la Kitope, Makame Mbarouk Mashimba, (CCM), alisema kwamba Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa ikipoteza haki zake ndani ya muungano kutokana na wabunge kutoka Zanzibar kuwa wazito kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya bunge hilo.
  “Mheshimiwa Mwenyekiti siyo kama nawageuka wenzangu tumewachagua kwenda kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano lakini wameshindwa kufanya kazi kusimamia haki na kutetea maslahi ya Zanzibar,” alisema Mshimba.
  Alisema kwamba wakati umefika Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waruhusiwe kuingia katika Kamati ya pamoja ya kujadili kero za muungano ambayo hukutana chini Mwenyekiti wake Makamu wa Rais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ili kuongeza nguvu za utatuzi wa kero za muungano.
  Hata hivyo, haliwataka wananchi wa Zanzibar kutumia vizuri fursa ya kutoa maoni juu ya katiba mpya ya muungano wakati ukifika kwa kuhakikisha wanatoa maoni yao bila hofi na kujiepusha na vitendo vya fujo na jazba ili kuhakikisha haki za Zanzibar zinazingatiwa katika mabadiliko hayo.
  Upande wake Mwakilishi wa Viti maalum (CCM) Asha Bakari Makame, alisema kwamba wakati umefika nafasi tano za Wabunge kupitia Baraza la Wawakilishi zifutwe kwa vile wabunge wanaonufaika na nafasi hizo wameshindwa kutetea maslahi ya Zanzibar bungeni.
  Naye Mwakilishi wa jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadhi Salmin, (CCM) na Mjumbe wa kamati Kuu ya chama alisema kwamba wabunge kutoka Zanzibar bado hawajafanyakazi ipasavyo katika kutetea maslahi ya Zanzibar, katika muungano.
  Naye mwakilishi wa Jimbo la Mkoani (CUF) Abdalla Mohammed Ali alitaka SMZ kutoa maelezo imekuwa ikinufaika vipi na Taasisi na Mashirika ya Umma ya serikali ya muungano ambayo yanatoa huduma Zanzibar.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zanzibar haihitaji support kutoka kwa Wabunge kumi waloko kwenye Bunge la Tanganyika, ni Wawakilishi kusema tu Muungano is Enough basi, Bunge la Wananchi wa Zanzibar ni Baraza la Uwakilishi Zanzibar BLW wao ndio wenye sauti Power kwa maslahi ya Wananchi wa Zanzibar.

  Laa Mukishindwa kufanya hivyo Ibara ya 10 ya Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar inaruhusu Wazanzibar kupiga kura ya maoni(Referendom) na kuamua hatma ya nchi yao.
   
 3. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,874
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  vilaza tu hao.. Wao kama wawakilishi wanauwezo wa kwenda hatua kubwa mbele pasipo kutegemea hao wabunge 10
   
 4. m

  mzaire JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wawakilishi ni mbumbu tu si waitishe kura ya maoni.
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Unafiki wa sitaki nataka ndiyo unaowasumbua hawa. Kwa mwendo huu wa kuwategemea Uamsho peke yake, kamwe hawatafikia malengo yao ya kupata zanzibar huru .
   
 6. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo Mshimba ni mwizi namba moja duniani, hajui hata kusoma wala kuandika, anaranda na mkalimani awatapeli wazungu kutwa,kila mwezi anapelekwa nje ya nchi na wahindi au wazungu ili wakanunue magari ni vitu vingine kwa jina lake ili huko avikomboe yeye bandarini waepuke kodi
   
 7. H

  Hute JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,044
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  MAKAME MBARUK MASHIMBA, yaani huyo ni jina la kisukuma kabisa, lakini anadiriki kuwatenga wasukuma wenzie wa bara akijiita yeye ni mzenji....kwani hao watu weuzi wa zenji walitokea uarabuni?...
   
 8. H

  Hute JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,044
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  yaani hao wote unawaona wamekaa kwenye vitu, utafikiri wana akili, kumbe wamebaki makopo matupu..hamna kitu hapo...ati wananyimwa haki..hivi ni haki gani ambazo wazenji na waislam kwa uujumla huwa wanaamini wananyimwa haki? hakiiiii hakiii haki gani jamani?
   
Loading...