juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,467
Bunge linaendelea,wabunge wa upinzani ambao ndio upande wangu wamezidiwa ujanja na CCM kabisa safari hii.yaani nimewadharau sana kwa kutoweza kulijua hili.
Hivi ni lini CCM waliungana na wapinzani pale bungeni katika kuamua jambo kwa pamoja? Eti safari hii wameazimia kwa pamoja hoja ya waitara kwamba Paul Makonda na Dc wa Arumeru waitwe kwenye kamati ya maadili ya bunge kwa kulidharau bunge.
Hivi nyie wabunge wetu hamjaweza kujitafakari kwa kina kwamba ni kwa nini ccm wakubaliane 100% na nyie?
Juzi Mh.Zito Kabwe si alitoa hoja binafsi kwamba bunge lijadili kwa nini wabunge wakamatwe hovyo wakiwa eneo la bunge? Je hao ccm walitoa ushirikiano?
Bunge live hakuna,wapinzani mlipaza sauti sana,je hao ccm walitoa ushirikiano?
Hakuna mikutano ya vyama vya siasa,mmelalamika sana je hao ccm walitoa ushirikiano?
Ni mambo mengi yenye tija kwa taifa huwa mnayapigania sana hadi wakati mwingine mnasusa na kutoka ndani ya bunge,lakini hao wabunge wa CCM hawajawahi kuwapa support. Iweje kwa hili wawe upande wenu?
Tena hili halina hata tija yoyote kitaifa.Hivi hili lina maana kuliko la katiba mpya? Mbona hawakuwasupport?
Yaani mmeshindwa kuelewa kwamba nyie mmefanywa kama daraja hapo? Daah,kweli akili ni nywele kila mmoja ana zake.