Chrisludos
Senior Member
- Oct 12, 2012
- 135
- 41
Na Chrisludos
Kwanza nianze kwa kuwapongeza wabunge wote wa upinzani waliofanikiwa kuchaguliwa licha ya changamoto mbalimbali walizokutana nazo.
Ni wazi uchaguzi wetu katika ngazi zote haukuwa huru na wa haki kwa wagombea kutoka vyama vyote.
Viashiria ni vingi kuwa tume ambayo ndio kama refa imekuwa ikipendelea sana wagombea wa chama tawala na kuwapa hali ngumu wagombea kutoka vyama pinzani.
Nadhani kile kilio cha miaka mingi cha kupata tume huru, hakipaswi kukoma kwani ndio njia pekee ya kukomesha uminywaji wa demokrasia nchini.
Lakini pamoja na changamoto zote hizo bado kuna jambo kubwa sana ambalo wagombea wa upinzani wanapaswa kujifunza kutoka kwa wale wa chama tawala.
Unaweza kujiuliza, Chenge anawezaje kupita kwa kishindo jimboni kwake pamoja na kashfa zote zinazomzunguka?
Tibaijuka anawezaje kurudi bungeni pamoja na dharau anazozionyesha?
Watoto wa viongozi kama Ridhiwani Kikwete, Godfrey Mgimwa na wengineo wanarithishwa majimbo na bado wanafanikiwa kushinda?
Mbunge anaongoza jimbo mpaka anachoka, kisha anamchagua anayemtaka yeye kulirithi jimbo na kweli anapita mfano Samwel Sitta na Mkewe Magreth Sitta, Membe na Nape na wengineo.
Lipo somo la kujifunza hapa, wamewezaje kujijengea ushawishi wa namna hii?
Mbona wengi bungeni wanasinzia na kuitikia ndiooooooo, basi wamemaliza.
Mbona wengi wana kashfa nyingi sana, wanawezaje?
Wakati huo huo wabunge machachali wa upinzani kama Kafurira, Machali, Wenje, Vicent Nyerere na wenginei wakikosa kurudi bungeni.
Na wale waliobahatika kurudi basi ni kwa mbinde, jaribu kuangalia jimbo la Mnyika, Mdee na wengineo.
Ni wachache waliopita kwa kishindo na tuliwategemea kama Mch Msigwa, Nassari na wengineo.
Ukweli ni kwamba wabunge wa upinzani wanatimiza wajibu wao ipasavyo kuliko wabunge wengi wa CCM, ila hawajui kula na kipofu.
Wanaweza kuwa wanatoa michango mizuri sana bungeni lakini hawajui kula na kipofu.
Wanazisaidia sana halmashauri zetu kuongeza mapato, pia kuzisimamia ziweze kuwahudumia wananchi lakini hawajui kula na kipofu.
Wanaibua ufisadi na kuisimamia serikali kwelikweli lakini bado hawajui kula na kipofu.
Wabunge wa CCM na wachache sana kutoka upinzani ndio wanaojua siri hii ya kula na kipo
fu ili kesho akupe kura.
Wananchi wengi wakitanzania hawajapata fursa ya kupata elimu, na hata walioenda shule pia hawajaelimika ipasavyo na hii ni kutokana na ubovu wa mfumo wetu wa elimu.
Wengi hawajui majukumu haswa ya mbunge, hawafatilii hata utendaji wa wabunge wao katika bunge na jinsi gani wanawajibika katika kuwaletea maendeleo katika majimbo na halmashauri zao.
Wabunge wa CCM wanawajua vizuri wapiga kura wao, ndo maana utakuta mbunge anaongoza jimbo kwa zaidi ya miaka 20 lakini bado yupo na ataendelea kuwepo.
Wanajua kula na kipofu, ni wasanii kwelikweli.
Wahudhuriaji na wachangiaji mashuhuri wa shughuli za kijamii kama misiba na sherehe mbalimbali.
Wengi wao wanajiweka na wapiga kura wao kwa kuwatembelea katika vijiwe au maeneo ya biashara kama masoko au stendi na kugawa hela na zawadi mbalimbali.
Pia utawakuta vilabuni na maeneo ya starehe wakigawa ofa kwa wapia kura wao.
Unaweza dhani ni wajinga, ila wameshajua wapiga kura wao wanataka nini na wao wanakula na kipofu kwani hawamshiki mkono, hawamshtui ila kila bunge na wao wamo.
Sisemi wabunge wa vyama vya upinzani waige yote hayo na kuacha kuwaletea maendeleo wananchi wao, hapana.
Walete maendeleo lakini pia wawe karibu na wapiga kura wao.
Utashangaa Joshua Nassari amerudi kwa kishindo bungenj licha ya kuongoza kwa kipindi kifupi, au Mchungaji Msigwa amepita kwa kishindo na kubeba kata nyingi safari licha ya kuingia kibahati 2010.
Lakini Mnyika au Mdee wamepata upinzani mkubwa jimboni mwao licha ya kuwa na umaarufu mkubwa.
Siri ni kuwa karibu na wapiga kura, kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kusambaza chochote ulichokifanya hata kama ni kidogo.
Kama wabunge wetu wa vyama vya upinzani hawatabadilika na kuwa karibu na wananchi wao, tutegemee kila kipindi cha uchaguzi kuanza upya kwa maana ya kuongeza majimbo wakati mengine yanapungua.
Mungu ibariki Tanzania.