Hawamtambui rais lakini walishiriki kupiga kura kwa ajiri ya kilicholetwa na rais wasiyemkubali, hiki ni kituko cha karne. Walimpinga rais lakini wakaomba wakafanye naye tafrija, kwani rais akiwa kwenye tafrija ndo haitwi rais? hiki nacho kinaleta kinyaa hatari. Hotuba ya rais kwanza ni lazima ijadiriwe bungeni, sasa sijui wanamaanisha hawatashiliki kuijadiri kwasababu hawamtambui rais, ama watashiliki kuijadiri hotuba wakati aliyeileta hawamtambui? haya yatakuwa maajabu ya dunia.
Tatizo la Ukawa naliona katika mambo yafuatayo
1. Wamegeuka wanaharakati.
2. Wanakosa watu makini wa kuwaongoza nje na ndani.
3. Utoto
4. Wameferi kutambua kwamba wao wanawakilisha majimbo yenye itikadi tofauti, wanahisi kana kwamba majimbo wanakotoka wananchi wote ni Ukawa na kwamba wanaridhia yanayofanywa na wabunge wao, wanajidanganya na matendo haya yatawaumiza zaidi wao kwasababu hata rais mwenyewe aliwaambia wananchi wapeleke watu ambao hawatakuwa na tabia za kususa na kutokatoka nje ..Ukawa wamekalia kuti kavu.