MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Magazeti ya leo yana habari inayosema wabunge wa tiketi ya CCM watakaoipinga bajeti ya mwaka huu wa fedha 2016/2017 wametakiwa na uongozi wa juu wa CCM na serikali kurudisha kadi za uanachama wa CCM ili wakaendeleze adhima yao kupitia tiketi za vyama vingine.
Uongozi wa juu wa CCM na serikali umesema mawazo ya wabunge kwenye mchango wa bajeti na michango mingine yatapokelewa na kufanyiwa kazi na serikali kwa maslahi ya taifa lakini wale wabunge watakaopinga kwa sababu ya maslahi yao binafsi hawawezi kuvumiliwa ndani ya CCM.
Uongozi wa juu wa CCM na serikali umebainisha kuwa hauwezi kuruhusu kuwepo bungeni na kundi lililojiandaa kukwamisha bajeti katika wakati huu ambao serikali imedhamiria kwa dhati kukuza uchumi na kufikisha huduma bora kwa wananchi hasa wa kipato cha chini kwa haraka zaidi.