Wabunge wa ccm nawauliza nani asiyetaka umaarufu wa kisiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa ccm nawauliza nani asiyetaka umaarufu wa kisiasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jun 30, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika historia ya Bunge letu mwaka huu na kipindi hiki cha Bunge neno 'wanatafuta umaarufu' limetumika sana. Na niseme kweli na mimi nimekwazika sana na maoni ya baadhi ya Wabunge hao kulitumia vibaya neno 'kutafuta umaarufu'. Labda tujaribu kutafuta maelezo yasiyo ya kitaaluma ya neno Maarufu, neno hili ni sifa chanya ya tabia njema ya mtu ambaye humpelekea kujulikana kwa watu wengi kwa wakati moja na si kujulikana tu bali idadi kubwa ya watu wanaomjua kwa wakati huo hujitokeza kuwa washabiki au wafuasi wake na hapa ndiyo chanzo cha gubu la kisiasa kwa wanasiasa ambao wanahisi umaarufu wao au taasisi wanayoiwakilisha inatishiwa na kukubalika na umma kwa upande mwingine. Hatari yake kisiasa ni kwamba umaarufu huo huenda pamoja na kupunguza mvuto wa upande mwingine. Sote tulitegemea kuwa mvuto wa CDM lazima kiwe kikwazo kwa wapinzani wake kisiasa na kwa hiyo kilio cha wabunge wengi kwa maandamano ya CDM hoja ya posho na hoja zingine bungeni sio tishio la amani bali tishio la mustakabali wao kisiasa.

  Labda niwakumbushe tu kuwa umaarufu hautafutwi na pia haupingwi jukwaani kwa bunduki au kwa kukataza. watu waliowahi kupata umaarufu kama vile wakina Nelson Mandela, Gadhi, Martn Luther King, Nyerere na wengine wengi hawa kulala siku moja wakajikuta ni maarufu, walijitofautisha na udhalimu, ufisadi, uonevu na kukaa upande wa wengi ambao walinyimwa haki.


  Wabunge Wanaokwazwa na utafutaji maarufu wa Wabunge wa CDM wasikae kwenye majukwaa au vipaza sauti vya bungeni kuwasema CDM watafute umaarufu ili wawe bora kuliko wenzao, tunachotaka kuwahabarisha ni kuwa umaarufu haununuliwi wala kuombwa bali ni matokeo ya kuishi maisha yaliyotukuka. Usimseme mwenzako kwa kutumia muda wake kusali kwani hiyo ndiyo njia aliyoichagua kumweka karibu na Mungu. Musiwakejeli wenzenu kwa njia zao walizochagua ili wawe karibu na waajiri wao kwani hiyo ndiyo salama yao. Mumenikumbusha enzi za shule mtu akisoma sana alipewa majina mengi mno mara Bundi, bookworm, mwanga nk yote haya hayakuwa na nia njema kwa msomaji bali kumkatisha tamaa ili asipate mavuno makubwa kielimu.

  siasa ni mbinu na mapambano waacheni wao wakejeli lakini tunajua shina limeanza kutikisika na wao wameona na sasa wanalilia ovyo hawana pa kushika

  ALUTA CONTINUAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
  VIVA MAANDAMANOOOOOOOOOOOOOO
  VIVA MAPAMBANO DHIDI YA POSHOOOO
  VIVA USHINDIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
   
Loading...