Jana ijumaa jioni ya 20/04/2012 na subuhi ya 21/04/2012 mbunge wa ngara, mh. Ntukamazina alijiunga na kambi ya akina zito akitaka baadhi ya mawaziri wang'olewe. Kilio chake si uchungu wa wizi uliofanyika. La hasha. Tegemeo lake ni kwamba wakin'golewa swahiba wake anaweza akampa uwaziri aliomwahidi wakati wa kampeni za 2010. Kama hii haitoshi, aliwataka madiwani wa ngara wawadhibiti watendaji wa halmashauri ya wilaya ya ngara. Ndugu zanguni, huyu mtu ni mbunge na pia kutokana na wadhifa wake ni diwani pia. Nani mwenye rungu kubwa - yeye au hawa madiwani ambao wamefulia ile mbaya yake baada ya kunyimwa viti kwenye meza ya ulaji?