Waziri wa Ulinzi, Dkt. Stergomena afungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi, wajadili Mwelekeo wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,966
BARAZA.JPG

Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Lawrence Tax ili afungue Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing).

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amefungua kikao cha Pili cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika katika Ukumbi wa Magadu Shirika la Mzinga Mkoani Morogoro.

Kikao hicho kimeendeshwa kwa mara ya kwanza kwa njia ya mtandao (zoom) ambapo Waziri alifungua kikao kutokea ofisini kwake Mtumba Mkoani Dodoma na wajumbe wakiwa Morogoro.

Agenda za kikao hicho ni kupitia Taarifa ya Mpango wa utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Mwelekeo wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na dondoo kutoka kwa wajumbe.

Taarifa hiyo iliwasilishwa mbele ya Baraza na Kaimu Kamishna wa Sera na Mipango, Alexander Allen Temu ambapo wajumbe walipata fursa ya kuijadili kwa kina na kutoa mapendekezo yao ambapo Mwenyekiti ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Muasilishaji mada waliweza kutoa majibu ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Dkt. Stergomena aliwakumbusha wajumbe wa Baraza lengo la kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi.

“Kama tunavyofahamu lengo la kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi mahali pa kazi ni kuimarisha utendaji kazi wa pamoja kati ya waajiri na wafanyakazi,” alikumbusha.
WAJUMBE.JPG

Wajumbe Wakishiriki Kikao cha Baraza la Wafanyakazi

“Shughuli mbalimbali zilizotekelezwa, baadhi ni pamoja na kulipa madeni mbalimbali ya wazabuni, kufanya tafiti, kulipa mishahara kwa wanajeshi, watumishi wa umma kwa wakati kulingana na stahili zao, kulipa posho ya chakula kwa Maafisa, askari na vijana wa JKT kufuatilia misamaha ya kodi na ushuru wa bidhaa.

“Kuendelea kutoa ushauri kwenye miradi ya ujenzi kwa Wizara na taasisi zingine, kufanikisha sherehe mbalimbali na maadhimisho ya kijeshi ya kitaifa, kutatua mogoro ya ardhi kwa kupima, kufanya tathimini na kulipa fidia kwa bbadhi ya maeneo,” alisema.

Aidha, Dkt Stergomena alitoa pongezi kwa wajumbe kwa kufanikisha utekelezaji wa majukumu hayo na Serikali kwa kutoa kipaumbele kwa sekta ya ulinzi.

“Nawapongeza sana sana kwa kazi nzuri iliyofanikisha utekelezaji wa majukumu haya. Aidha, naishukuru Serikali yetu kwa niaba ya Wizara inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya ulinzi na usalama,”

Dkt. Stergomena alitoa wito na kuwaomba wajumbe kusimamia na kuwahimiza watumishi kufanya kazi kwa weledi, kwa uadilifu na kuepuka ubadhilifu wa rasilimali za Taifa na kujilinda dhidhi ya magonjwa ambukizi na yale yasiyoambukiza.

“Napenda kuwasistiza na kuwaomba wajumbe kuwa wasimamizi wa mambo manne ambayo nitayataja hapa na kuahimiza watumishi kuyazingatia. Jambo la kwanza ni kufanya kazi kwa weledi, kufanya kazi kwa udilifu pamoja na uadilifu kazini, kulinda rasilimali za taifa letu pamoja na kujilinda na magonjwa hatari yakiwemo UKIMWI na UVIKO-19 na magonjwa mengine yasiyoambuza,” alisistiza.

KATIBU.JPG

Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, NEWA akimkaribisha Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe ili ahitimishe kikao.

Vikao vya mabaraza ya wafanyakazi ni utekelezaji wa takwa la kisheria ambalo chimbuko lake ni Tamko la Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere (Tamko Na. 1 la Mwaka 1970) na Sheria nyingine za kazi za nchi yetu na zile za kimataifa zinazohimiza ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kufanya maamuzi mbalimbali kupitia mabaraza ya wafanyakazi.

Aidha, Baraza hili ni jukwaa muhimu mahali pa kazi kwani ni kiungo kati ya Menejimenti na Wafanyakazi.
 
Back
Top Bottom