Wabunge mmemgomea Rais Magufuli?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Rais 'aliruhusu' kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kuhamasisha maendeleo majimboni. Rais Alisema kila Mbunge afanye mikutano katika jimbo lake. Afanye mikutano isiyo na utani kuhusu maendeleo kwa yake aliyoyaahidi.

Tangu 'ruhusa' hiyo itoke kwa Rais Magufuli, hapaonekeni mikutano ya kimaendeleo majimboni. Hakuna kuelezwa kwa wananchi juu ya kilichosemwa,kilichofanywa na kitakachofanywa na Mbunge husika jimboni mwake.

Je, Wabunge mmemgomea Rais kufanya mikutano ya kimaendeleo?

Mwafaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Wengi si tu wanamuogopa Magufuli, lakini pia wanaogopa mpaka kivuli chake.
Hasa kutoka kwenye chama chetu cha kijani.

Usitegemee kutafanyika mikutano kwenye mazingira kama hayo.
 
mitaani kutakuwa kama sokoni mbunge, mkuu wa wilaya,waziri, mkuu wa mkoa, wakurugenzi, wenyeviti wa vyama, madiwani lazima tuchanganywe na miluzi mingi
 
Ni mgomo baridi, kisa kutokuwepo posho za vikao! Wafwaaa!
 
Wabunge kuwaona machoni petu huku wakiwa wanaogopa kutamka neno njaa ni ishara ya dharau kwa wapiga kura
 
Wanaogopa kukamatwa inawezekana kusingiziwa kuwa wanaleta uchochezi wa kisiasa kwenye hiyo mikutano ya hazara ya maendeleo
 
Rais 'aliruhusu' kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kuhamasisha maendeleo majimboni. Rais Alisema kila Mbunge afanye mikutano katika jimbo lake. Afanye mikutano isiyo na utani kuhusu maendeleo kwa yake aliyoyaahidi.

Tangu 'ruhusa' hiyo itoke kwa Rais Magufuli, hapaonekeni mikutano ya kimaendeleo majimboni. Hakuna kuelezwa kwa wananchi juu ya kilichosemwa,kilichofanywa na kitakachofanywa na Mbunge husika jimboni mwake.

Je, Wabunge mmemgomea Rais kufanya mikutano ya kimaendeleo?

Mwafaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Walifanya UPINZANI wameishia LUPANGO??Labda alimaanisha kwa Wabunge wa CCM.Hapa nasikiliza tu DARASA napata majibu.
 
Ukienda kuomba kibali polisi unaishia kuambiwa kuwa intelijensia yao imeona kuwa kutakuwa na uvunjifu wa amani hivyo imezuia kibali!! Mfano: Chama cha CUF mikoa ya kusini alipowatembelea Maalim.
 
Back
Top Bottom