Wabunge kuungana bunge la bajeti 2017/2018

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,944
Kwa mtazamo wangu natumaini wabunge wataondoa tofauti zao za kisiasa katika bunge la bajeti 2017/18 kwa sababu zifuatazo;

1. Baada ya bajeti iliyokuwa ikinadiwa na waandishi wa habari kwenye televisheni,magazetini,redio na vyombo vingine kuvurugwa na kutokutatua changamoto wa mlalahoi.

Bajeti hii ilionyesha usaliti wa wazi wa wabunge kwa wananchi wao ili tu wamrizishe Mheshimiwa na kuikomoa kambi ya upinzani.Naamini watajutia kosa na kuitazaza Tanzania na si CCM wakati wa bajeti ijayo.

2. Wabunge wataamka na kugundua kuwa wananchi ndio waliowatuma. Hapa nazungumzia hasa wale waliopita kwa kujinadi kwa kuomba kura.Muda unakwenda na wakati wa kupeleka mrejesho kwa wananchi 2020 katika uchaguzi mkuu na 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa, wananchi wanaoelimika wasiodanganyika kwa sera mfu za kizamani za kuwaambia wachague chama fulani kimeleta amani kwa miaka mingi huku wakiambiwa ukichagua mkono mwingine kwamba yatatokea machafuko huku huelezei kivipi hayo machafuko yatatokea.Hakuna mwenye akili aliye tayari kuona hali ngumu katika jimbo lake kwa kumwabudu mtu mmoja.

Nawaomba vijana tujitokeze kwa wingi 2019 katika kuwania nafasi serikali za mitaa na 2020 ili kuleta uwakilishi chanya kwa wananchi.
 
Kwa mtazamo wangu natumaini
wabunge wataondoa tofauti zao za kisiasa katika bunge la bajeti 2017/18 kwa sababu zifuatazo;
1:Baada ya bajeti iliyokuwa ikinadiwa na waandishi wa habari kwenye televisheni,magazetini,redio na vyombo vingine kuvurugwa na kutokutatua changamoto wa mlalahoi.
Bajeti hii ilionyesha usaliti wa wazi wa wabunge kwa wananchi wao ili tu wamrizishe Mheshimiwa na kuikomoa kambi ya upinzani.Naamini watajutia kosa na kuitazaza Tanzania na si CCM wakati wa bajeti ijayo.
2.Wabunge wataamka na kugundua kuwa wananchi ndio waliowatuma,hapa nazungumzia hasa wale waliopita kwa
kujinadi kwa kuomba kura.Muda unakwenda na wakati wa kupeleka mrejesho kwa wananchi 2020 katika uchaguzi mkuu na 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa, wananchi wanaoelimika wasiodanganyika kwa sera mfu za kizamani za kuwaambia wachague chama fulani kimeleta amani kwa miaka mingi huku wakiambiwa ukichagua mkono mwingine kwamba yatatokea machafuko huku huelezei kivipi hayo machafuko yatatokea.Hakuna mwenye akili aliye tayari kuona hali ngumu katika jimbo lake kwa kumwabudu mtu mmoja.
Nawaomba vijana tujitokeze kwa wingi 2019 katika kuwania nafasi serikali za mitaa na 2020 ili kuleta uwakilishi chanya

kwa wananchi
Wabunge wa upinzani wakati wa bajeti wanataka nje kama kawaida
 
Hicho unacho kisema hakipo kabisa kwa wabunge wa CHAMA CHA MAPINDUZI hawa walio ungana kuikataa katiba ambayo ndiyo ingekuwa chachu ya maendeleo kwa kuondoa baadhi ya ujinga wa katiba ya 1977 !? labda unaongelea wabunge wengine , lakin kama ni wa chama cha CCM usitegemee hilo ,wabunge wa chama hiki wengi wao ni wajinga kabisa na hawajui hata wajibu wao kwa wananchi wao , wao wanaamini kuwa pale walipo ni halali yao na haki yao wakati wamesahahu kuwa wananchi wamewatuma wakawawakilishe ila ni baadhi si wote na miongoni mwao naomba kwa dhati kabisa nimtoe BASHE kwenye kundi hilo na RIP . D.FILIKUNJOMBE. wengine wenye utimamu na ufahamu wa akili bado tuendelee kuwatafuta ndani ya kundi hilo la tope.
 
Wabunge wa CCM ni wanafiki sana, wakiona mambo yanazidi watajifanya kuungana na wale Critical thinkers from OPPOSITION. Ni waoga na ni wanafiki Sana
 
Budget hii (2016/17) ni ya Ovyo sana...

Walipitisha makodi ya ovyo ya kuuwa Uchumi.....VAT kwenye tourism

Natumaini safari hii Waziri Mpango hutadanganywa tena na wakenya....Manyang'au walimdanganya waziri ili kuua utalii wa Tanzania....Sabotage Tanzania economy...

Shillingi imeanguka thamani kwa sababu watalii wamepungua au wamepaki namba ile ile (remain dormant..constant) badala ya kuongezeka.

Bandarini wameongeza kodi na mizigo imepungua

Safari hii wabunge simamieni masilahi ya Taifa
 
Wanapiga deal la 10%...midege mibovu....unanunua dreamliner kwa 500 billion...fedha ingewekwa kwenye miradi ya maji wakina mama wangetuliwa ndoo...wanawake wa Tanzania CCM haiwajali ..mtakunywa maji na mifugo mpaka lini?
 
Kuliko kununua ndege na umeua utalii na uchumi...bora angejenga miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji

Kuza uchumi na kipato cha mwananchi....kwanza..Then ndege zije baadae

Ndege- watalii hakuna --VAT na kipato cha wananchi duni..

Sasa hivi ni njaa ..njaaa

Ajira hakuna
 
Wanapiga deal la 10%...midege mibovu....unanunua dreamliner kwa 500 billion...fedha ingewekwa kwenye miradi ya maji wakina mama wangetuliwa ndoo...wanawake wa Tanzania CCM haiwajali ..mtakunywa maji na mifugo mpaka lini?
CCM ina jeuri kweli.Mito mikubwa na maziwa yote haya bado watu wanakunywa maji yaliyotuama ya mvua
 
Watalipwa vichenji na kamchezo kataishia hapo hasa hawa wa ccm km ule muswada wa habari ulivyopita kwa rushwa ya milioni kumi kwa kila mbunge wa ccm km tulivyoambiwa.....hahahaaa kanchi kaabunuwasi bwana......kanaendeshwa kiabunuwasiabunuwasi....ccm hawana uchungu kabisa mbele ya pesa.....afadhali ukose mali kuliko kukosa fikra sahihi.
 
Jua muda ukifika mtasogeza goli mpaka 2025,ni kawaida.

Mwaka juzi ilisemekana CCM hawatoki
 
Back
Top Bottom