Artery
Member
- Jul 11, 2015
- 67
- 52
Nimekuwa nikiliwaza hili la Rais kuwa na nafasi kumi za kuteua wabunge... wakati wa JK nililiona haka ni kauchochora kakupitisha mabest na mashost wa rais, ilikuwa ni nafasi ya rais kuwapa watu ulaji, anateuliwa kuwa mbunge, anaenda kukaa mle ndani ya mjengo anakula kiyoyozi na posho juu miaka mitano ikiisha anarudi mtaani amenawiri, anasubir kuteuliwa tena au anatafuta jimbo la kugombea.. baada ya JK kubanwa mara kwa mara nakulazimika kuvunja baraza la mawazir kidogo akaanza kubadilisha upepo, anatuea kuwa mbunge then anampachika uwaziri...
Awamu hii mambo yamenoga zaidi, unateuliwa mbunge, kabla hata hujaapa kuwa mbunge unapigwa zigo la uwaziri... hili naliona ni jambo jema kwa upande mmoja, kuwa Rais anapata nafasi ya kutoka nje ya boksi na kutafuta yupi hasa anaweza kumsaidia kwenye serikali yake hata km hajatoka jimboni!!!
Lakini pia linakuja swala tata la wabunge wetu wanaotoka majimboni, kwamba awamu hii JPM amechunguza kapu la wabunge mia mbili na ushee wa CCM kajikuta inabidi aimport watu wengine ndo awape wizara nyeti serikalini, kwamba waliopo wengi hawafai kuwa mawaziri, kwamba huko majimboni wanapita watu ambao hawawezi kusaidia serikali yetu katika nafasi nyeti... hapo ndipo unapoona kuwa katiba yetu ina shida, ili uwe mbunge minimum qualification uwe unajua kusoma na kuandika, yaani angalau elimu ya msingi...
Upande wa pili linakuja umuhimu pia wa labda kutenganisha ubunge na uwaziri, kwamba ili uwe wazir lazima uwe mbunge, hili nalo linahitaji kuangaliwa upya kwa sababu linaleta mgongano, Rais analazimika kuchagua mawaziri ktika sample ya wabunge, hata km hawana ubora wa kutosha inambidi ateue tu, kwa sababu hata sasa ungemwuliza JPM kuwa katika wale mawaziri aliowateua je ni kweli kwamba ndo kaona wanafaa au imembidi tu achukue hata km hawatafit kwenye hizo nafasi, maana tayari hata angeona wengine huku nje, ni nafasi kumi tu anazo za kuteua, zinazobaki lazima arudi kwenye kapu la wabunge waliopo..
Nionavyo huu ni utata mkubwa wa kikatiba, huku inahitaji mbunge awe na minimum qualification ya kusoma na kuandika huku inalazimisha mawaziri watokane na wabunge, obviously unatengeneza serikali dhaifu sana tena sana...maana hata hao wabunge ni watunzi wa sheria zetu... ndiyo maana ndiyo hazitaisha kwenye bunge zetu!!!!