Geeky
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 307
- 181
Mbunge CCM amponda rais
BAADHI ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wameipinga hotuba ya Rais Kikwete kwa madai kuwa imejaa vitisho na kujibu hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba.
Mmoja wa wajumbe aliyezungumza na Tanzania Daima Muda mfupi baada ya kumalizika kwa hotiba ya Rais Kikwete katika uzinduzi wa Bunge Maalumu la Katiba, Kangi Lugola, alisema kuwa kauli ya Kikwete ni matokeo ya ukiukwaji na uvunjwaji wa kanuni.
Alisema imesikitisha kuona rais akiwa na sura ya vitisho na kwa wajumbe wa bunge maalumu huku akiwa anaibeza rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Jaji Warioba.
Kwa upande wake mjumbe wa Bunge la Katiba, Maria Sarungi alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete imechukua muda mrefu na kujiondoa katika hotuba na badala yake kuwa kama semina.
Alisema pamoja na mapendekezo yake ya kutaka kuwepo kwa muundo wa serikali mbili, haiwazuii wajumbe wa Bunge Maalumu kujadili na kupendekeza maoni yao ambayo wanaona yanafaa.
source:TanzaniaDaima.