commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,954
Wana bodi,
Mh Andrew chenge, mbunge wa jimbo la bariadi, mkoa wa simiyu.
Si Jina geni katika siasa za Tanzania. Kwa ufupi ni mmoja wa viongozi waandamizi katika siasa za nchi hii. Tangia awamu mbili nyuma.
Lakini alijizolea umaarufu zaidi kwa kashfa ya chenji ya rada, katika awamu ya Mh, Benjamin William mkapa...
Tangia hapo na hadi sasa hajawahi safishika kamwe
Kwa maana kwamba iwe ni rada au escrow, hakuna tofauti Kati ya Chenge na Edward ngoyai Lowassa. Wote ni watuhumiwa ambao kamwe bado hawsjasafishika mbele ya watanzania walio wengi wachukia ufisadi, na wapenda maendeleo ya nchi yetu.
Kama CCM, na watanzania kwa walio wengi tumemhukumu lowasa, Kulikoni chenge?
Na pia hata kimataifa, watu au Jina la chenge bado liko kwenye rekodi ya mafaili makosa ya rushwa kubwa kubwa kuwahi kutokea nchini.
Sasa uongozi wa serikali ya awamu ya tano, umeingia ikulu ya magogoni kwa kauli mbiu ya` hapa ni kazi tu`
Pia Mh JPM, akijitahidi kutumbua majipu kadri ya uwezo wake (MUNGU amjaalie).
Sasa nyinyi wabunge wa CCM kwa kutumia wingi wenu bungeni, mmemchagua Andrew chenge. Kushika nafasi nyeti ya Mwenyekiti wa bunge kumsaidia Mh spika wa JMT.
Napenda muelewe kwamba mmewachanganya sana watanzania na si hivyo tu, Bali mmemuweka hata Rais mwenyewe katika mazingira magumu katika kusimamia kile ambacho anakiamini yeye katika vita hii dhidi ya maovu., ili kutimiza azma yake ya hapa ni kazi tu, na pia kutumbua majipu, kwa sababu itafika mahali atashindwa kutimiza wajibu wake bila kugongana kimfumo na mihimili mingine. Muhimu kikatiba.
Kwa kitendo Chenu hiki, pia mnafanya taswira ya mheshimiwa magufuli kimataifa, katika taswira ya kupambana na ufisadi ififie, kwani wataona kama bado na yeye ni sehemu ya wao!
Ndio maana nimewauliza, Je hamkuona wengine zaidi ya Chenge?
Je mtakuwa tayari kwa mfano Rais yuko katika ziara kikazi nchi za nje anakumbana na swali kama hili..
Mh Rais JMT,
Ulipoingia madarakani, baada ya Uchaguzi, ukiwaahidi watanzania na Dunia kwa ujumla, kwamba utaunda serikali, yenye kufuata miiko ya uongozi na uwajibikaji wa pamoja,
Yenye kuuchukia ufisadi.
Yenye kuwajali raia na kuwatatulia kero zao nk.
Je Mbona baadhi ya mihimili nyeti kama bunge, tunaona uteuzi wa baadhi ya watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wakichukuwa nafasi muhimu kimaamuzi?
Je hili si kikwazo kwa mhimili huu nyeti kitaifa, pale utakapohitaji kupata usaidizi wa karibu toka katika chombo husika..
Je waheshimiwa wabunge mlitafakari kabla ya kuamua?
Kama mlitafakari, Je mlikumbuka kwamba kuna Uchaguzi mwingine ifikapo 2020?
Je mtakuwa na utayari wa kutupiliwa mbali na wapiga kura wenu?
Tunatarajia wabunge mumsaidie JPM kutatua kero za wananchi, Je ni kweli mko nae kimawazo na kivitendo?
Hili ni jukwaa huru, naomba wenye yao moyoni nanyi mtupie hapa.
Nawasilisha.