Waandishi wa habari acheni uwoga

Tagawa Mwakitombile

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
462
386
Huwa nikobored pindi nisomapo gazeti na kukuta maneno haya
mtuhumiwa huyo...(jina tumelihifadhi)

ambaye anamiliki kampuni iitwayo..(jina tumelihifadha)

then baada ya majuma kadhaa hutasikia habari hiyo ikiandikwa tena yaani kwa kifupi huwa inatupiwa kapuni especially kama tuhuma hizo zinamuhusu kigogo sasa kama ndo hivyo kulikuwa na ulazima wowote wa kutujuza habari ya dizaini hii? Ambazo zinaniacha mm msomaji na alama za viulizo


Kwa mm ninavyofahamu kama unaushahidi hunabudi kumtaja jina huyo muhusika so kwa hali hii inanitia mashaka na kunifanya nijiulize maswali je hawa waandishi wa habari huwa wanakurupuka pindi waandikapo habari zao?

Kama sio mbona hali hii ya (jina tumelihifadhi)
haiwatokei makabwela?


Naomba mbadilike (waandishi wa habari) msiandike habari kwa kufuata itikadi yoyote ile#
 
Back
Top Bottom