Waandamaji Mali wakijivinjari Ikulu

Waandamaji Mali wakijivinjari Ikulu

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
535691_107260909413091_100003875460463_39294_59356247_n.jpg


Baada ya JF kunizingua, niliamua kwenda zangu Mali kutembea nikakutana na peoples power wa huko wakiwa wanajivinjari Ikulu baada ya kumpa kichapo Rais wao hadi kuzirai. Mamia ya waandamanaji hao walimshambulia Rais Traoure wakipinga mkataba ulioafikiwa na Tume ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, ECOWAS, ambapo Traoure ataendelea kutawala kwa hadi mwaka mmoja badala ya siku 40 pekee zilizokubaliwa miezi miwili iliyopita.

Wakuu wa serikali nchini Mali wamesema kuwa Rais huyo wa Mpito amepelekwa eneo salama baada ya kupigwa hadi kuzirai na mamia ya waandamanaji. Wanajeshi waliwaruhusu baadhi ya waandamanji kuingia katika ikulu ya rais ingawa bwana Traore hakuwepo wakati huo.

Shambulio hilo limewashtua wanadiplomasia waliokuwa wakifanya kila juhudi kurejesha amani na utangamano nchini humo. Muda wa kuongoza aliopewa Traore ulitarajiwa kukamilika Jumatatu. Lakini viongozi wa nchi za Magharibi mwa Afrika, waliafikia mkataba na kiongozi wa mapinduzi Kapteni Amadou Sanogo kwamba Bw Traore asalie mamlakani ili aweze kuongoza harakati za uchaguzi na kumaliza harakati za waasi wa Tuareg.

Mkataba huo pia ulijumuisha mpango wa kukubalia Sanogo atajwe kama kiongozi wa zamani alipwe mshahara wa rais na apewe nyumba ya kifahari. Mapinduzi hayo pamoja na harakati za waasi kuteka Kaskazini mwa Mali, yamesababisha maelfu ya watu kutoroka makwao. Mashirika ya misaada wanasema wana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Mali nchi ambayo pia inakumbwa na baa la njaa.
 
Wananchi waliingia Ikulu Kama wanaingia sokoni. Inaonesha jeshi, polisi na wanausalama Kama sehemu ya Raia hawamtaki kibaraka aliyewekwa.
 
Ni baada ya kuchoshwa.. Nadhani Ecowas na jumuia ya kimataifa haikuwatendea haki wananchi wa Mali kwa kuwarudishia raisi yule yule alieondolewa madarakani.. eti awaongoze kwenye kipindi cha mpito.. At least wananchi wa Mali wameonyesha kwa vitendo hasira yao..
 
Nami nina hamu ya kwenda kujivinjari magogoni..... sijui lini wananchi wenzangu nasi tutachoma ndani pale jumba jeupe....
 
tusiongee kama makasuku tusiowezaq analyse issues, huyu ndie rais aliyeshinda uchaguzi wa halali baada ya wanajeshi kubanwa na jumuia ya kimataifa na kutishiwa kijeshi na kimisaada kumrudisha ndio wamemrudisha lakini wamefanya mcehzo mbaya wa kuandaa wahuni wakamvamie na kumpiga ili ionekane kua hapendwi na wananchi, wafuasi wake ambao ndio wananchi wengi wanaogopa kujitokeza mitaani, rais huyu hana uwezxo hata wa kufanya mabadiliko yoyote so wanajeshi wanamtishia ili ahame nchi au aseme mwenyewe kua hataki urais, uliona wapi watu wanavamia ikulu na hawaogopi chochote na walinzi hawawakamati! ni game imechezwa very shameful!
 
hahahahaaaa....nimeipenda. jamaa kaingia na bodaboda.
 
hahahahaaaa....nimeipenda. jamaa kaingia na bodaboda.

Yaani mkuu hiyo ndio imenimaliza kabisa. Huyo jamaa kaona ujinga huu ngoja nitinge na bodaboda ndani ya jumba jeupe. Hivi mtu unapigwa na wananchi hadi unazimia bado tu una hamu ya kuendelea kuwa madarakani? Wakirudi tena watamgawana akiwa hai!

Naona kama Cpt. Sanogo aliwaachia kidogo wampe nidhani huyo Rais wa ECOWAS!
 
Back
Top Bottom