Waamuzi wanaziogopa Simba na Yanga

Waamuzi wanaziogopa Simba na Yanga

man dunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2013
Posts
3,877
Reaction score
6,902
Pamoja na waamuzi waliochezesha mechi ya simba na yanga iliyofanyika jumamosi kuimudu kwa asilimia kubwa lakini kuna maamuzi yalifanyika ambayo yaliniacha nijiulize maswali.Maamuzi yenyewe ni kuongeza dakika tatu tu baada ya dakika tisini na kumaliza mechi kabla dakika za nyongeza kumalizika. Kwa aliyetazama pambano hilo atakubaliana na mimi kwamba pambano lilisimama zaidi ya dakika kumi kutokana na tafrani ya taulo na kipa ivo mapunda kupatiwa tiba baada ya kuumia. Sasa kwa nini dakika tatu tu? Je waliogopa kuwa wakiongeza zaidi timu moja inaweza fungwa na kwa hiyo watalaumiwa na aliyefungwa? Vilevile kitendo cha mwamuzi kumaliza mechi kabla ya dakika tatu, je mwamuzi aliogopa shambulizi lililokuwa linafanywa na simba kwamba lingezaa goli na yeye kuweza laumiwa?
 
hata me nimeshangaa kuona zinaongezwa dakika tatu tu wakati game ilisimama kwa muda mrefu. kama ziongeongezwa dakika saba hawa simba tungewalaza goli lingine coz ulinzi wao (taulo) ulikuwa umeondolewa
 
Back
Top Bottom