Wa mikoani.

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,863
Habari zenu wana bodi;

Imekuwa jambo la kawaida kwa wakazi wa dar kuita nje ya dar mikoani.

Je! dar ni wilayani, kwahiyo nje ya dar ni mkoani???

Bado sijaelewa nini mantiki ya hilo neno.

Naombeni ufafanuzi tafadhali...
 
Mbona hata wakazi wa arusha huita mikoa mingine mikoani, usipotoka arusha watu watakuita wa mkoani,
Kwa iyo si wa dar tu ni mkoa wowote ule.
Fanya research yako vizuri
 
Ok:

Vipi mantiki ya huo msemo???
 
Habari zenu wana bodi;

Imekuwa jambo la kawaida kwa wakazi wa dar kuita nje ya dar mikoani.

Je! dar ni wilayani, kwahiyo nje ya dar ni mkoani???

Bado sijaelewa nini mantiki ya hilo neno.

Naombeni ufafanuzi tafadhali...

Dar ni jijini, Arusha pia ni jiji, hivyo kuna tofauti kati ya jijini na mkoani.
 
Kwahiyo dar sio mkoa???

Mbona katika idadi ya mikoa Tanzania , dar na arusha zimo????
 
mimi mtu akishasema ooh nilisafiri nilikwenda mkoani sijui huwa namuonaje!! hana tofauti na wale wanaosema nimekudeep lakini hukupokea yaaani aghhhh!!! watanzania wengi ni wajinga hatupendi kujifunza vitu vipya.
 
Huwa nashindwa kuelewa mantiki ya hili neno.

Hili neno " nimekudeep" linanikera sana.
 
mimi mtu akishasema ooh nilisafiri nilikwenda mkoani sijui huwa namuonaje!! hana tofauti na wale wanaosema nimekudeep lakini hukupokea yaaani aghhhh!!! watanzania wengi ni wajinga hatupendi kujifunza vitu vipya.

ni kawaida tu tulishaga jizoelea wenyewe na misemo hiyo na tunajivunia kuwa watu wa mikoani mfano mi nipo Iringa niitwa wa mkoani mi naona poa tu maisha yanasonga tu hamna noma
 
MWANAKA

Mimi nimeshindwa kuvumilia. Mimi nipo Kilimanjaro, unakuta jamaa ananiita wa mkoani. kwani ye wa Wilayani???
 
Last edited by a moderator:
nimeshawahi kumnasa mtu vibao kwa kauli hii.
unataka kujua wapi huko?
(gugo,Ngwinde!)

y-n
Hiyo kesi uliimaliza vipi???
 
Last edited by a moderator:
Dar es Salaam ni mkoa kama ilivyo mikoa mingine unaoufanya jumla ya mikoa iwe 25 kwa Tanzania Bara au 30 ukijumlisha na mitano ya Zanzibar.

Matumizi ya neno 'mkoani' kama lilivyozoeleka kwa wakazi wengi wa Dar es Salaam wakimaanisha eneo lolote la nchi nje ya Dar es Salaam, kwa mtazamo wangu sio sahihi hata kidogo. Ni dhana potofu ambayo kwa sehemu kubwa imebeba maudhui kuwa dar es salaam ni 'bora' (soma ina hadhi) kuliko maeneo mengine. Ni mwendelezo wa utamaduni na kasumba ya baadhi ya watu au kundi fulani kujiona wao ni bora kuliko wengine katika jamii iwe kwa sababu za kiuchumi, kiografia, kijamii au nyinginezo. Siupendi msemo huo, nasema tena siupendiiiiiiiii!!!!!!

Habari zenu wana bodi;

Imekuwa jambo la kawaida kwa wakazi wa dar kuita nje ya dar mikoani.

Je! dar ni wilayani, kwahiyo nje ya dar ni mkoani???

Bado sijaelewa nini mantiki ya hilo neno.

Naombeni ufafanuzi tafadhali...
 
ni kawaida tu tulishaga jizoelea wenyewe na misemo hiyo na tunajivunia kuwa watu wa mikoani mfano mi nipo Iringa niitwa wa mkoani mi naona poa tu maisha yanasonga tu hamna noma

hakuna mtu ambaye hayupo mkoani bana, tuwe tunawaelimisha wenzetu, hivi unajua kuna watu tena wengi tu hawafahamu kama hata dar ni mkoa
 
Dar?Dar ni mji mkuu wa Tanzania na Dodoma n makao makuu ,Ninyi wa mbeya,iringa,kilimanjaro,sijui wapi simiyu wote ni wamikoani tu,Ninyi wa ..ee.. bac msije mkanipiga makofii..amkawii ninyi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…