Nakuwa mvivu kusoma postings ndefu lakini hii nimesoma hadi nukta ya mwisho maana inanihusu. First born.
Mkuu wakati mwingine ni mtihani kweli hasa mkiwa wengi wa mama tofauti. We acha tu. Tenda wema uende zako. Madogo unawasomesha kama ulivyosema wakianza kazi ndio utajua kama muhogo ni chakula au futari.
Niwatakie jioni Njema wanajamii, wakati huu mkiwa ktk harakati za kumaliza kulitumikia taifa jioni hii, hebu ongeza kidogo ktk maarifa yako.
Kama wewe ni FIRST BORN! Hii inakuhusu:
Hii ni kwa wale waliotanguliwa kuzaliwa, lugha nyepesi ni kuwaita wa-kwanza kuzaliwa, katika familia zao, lakini pia inawahusu na walio zaliwa wa-pili. Katika namna nyingine, hii hali huwa inawagusa hata wa-tatu kuzaliwa. Kimsingi ni kwamba, kwa jamii yetu, ktk zile familia za kati na za chini kiuchumi, hutokea kwamba watoto tajwa hapo juu, huzaliwa wakati wazazi wakiwa ktk "neema", ama kurahisisha niseme watoto tajwa huzaliwa wakati familia hizi zipo ktk piki!
Watoto hao huzaliwa katika kipindi ambacho:
- Baba na mama wapo ktk kilele cha mafanikio (inawezekana kipato ama mapenzi)
- Baba na mama wapo ktk maelewano ya hali ya juu
- Baba na mama wapo ktk rika lao la ujana, wakiwa na nguvu nyingi, zikiwemo za kufanya kazi (ama biashara), akili n.k
- Baba na mama wakiwa hawana aina anuai za migogoro!
- Baba na mama wakiwa ktk kusikilizana kwa mipango mingi, na hasa inayohusu ujenzi wa familia!
Kwa kuzingatia dondoo hizo 5, inategemewa kuwa watoto waliopatikana katika mazingira haya, kuwa hufaidi sana rasilimali za familia husika.
Hiki ndio kipindi ambacho mtoto atapatiwa mahitaji ya aina nyingi kadri wawezavyo wazazi. Mtoto katika hali hii atapata mahitaji ya lazima na yasio ya lazima. Si wazazi wanapambana kadri ya uwezo wao wote!
Hiki ndio kipindi mama atahudhuria klinik bila kukosa. Mama hana raha kuwepo ofisini kwa vile akili ipo kwa mtoto, ndio hapa ambapo mtoto hata akiumwa mafua, mbio hospitali, mtoto hajalala, simu kwa mume, mtoto kachelewa kuamka mama roho juu! Mtoto kacheua, simu kwa daktari, mtoto kalala na kuamka bila kukojolea nepi, simu kwa dr!
Baba nae hivo hivo, juice za kila aina, midoli, muda wa kucheza na mtoto unatengwa, bajeti ya ziada itakuwepo kwa ajili ya mtoto huyu, madawa baridi ya mtoto yatajaa kabatini n.k!
Kifupi ni kwamba, haiwezekani watoto wa ainaa hii kukulia ktk dhiki ama hali ngumu (mara chache hutokea). Kadri miaka inavokwenda, aina hii ya malezi hupungua kutoka mtoto wa kwanza, mpaka wa pili, na pia kutoka mtoto wa pili mpaka wa tatu, utaratibu huenda hivo mpaka mtoto n[SUP]th [/SUP]kuzaliwa. Hatupaswi kulaumu. Mengi hutokea hapa kati kati.
- Kuna kuyumba kiuchumi kwa wazazi
- kuna kuachishwa kazi
- kuna kustaafu kazi
- kuna kuyumba kwa biashara ama kufilisika
- kuna kuongezeka kwa majukumu ya familia mfano ujenzi wa nyumba ama ununuzi wa gari (gari huja na aina mpya ya matumizi, mafuta, vipuri, n.k)
- kuna ada za shule (hii huwaathiri 2[SUP]nd[/SUP] born ama 3[SUP]rd[/SUP] born) n.k
Kama ukweli ndio huu basi, inabidi tupate mafunzo haya:
- kama wewe ni 1[SUP]st[/SUP], 2[SUP]nd[/SUP], 3[SUP]rd[/SUP] ama mkubwa wa familia yenu, kuwa tayari kujitolea uwezavyo kwa wale wa nyuma yako.
- Jitolee kwa kuwa wale ni ndugu zako, sawa, jitolee zaidi kwa kuwa wewe ulifaidi "family cake" zaidi kuliko wadogo zako.
- Wewe ulizaliwa wakati wa neema za baba na mama, wapo wadogo zako labda walikuta kuna kupungua kwa neema ama zilishaisha kabisa, inawezekana wewe ndio ulieambiwa usiende Govt sec school na wazazi, kisha wakakupeleka shule nzuri ya binafsi kwa elimu bora, leo wazazi hawana uwezo huo kwa wadogo zako!
- Mke ama mume wako asiwe kikwazo cha wewe kuwasaidia waliokuja nyuma yako, nduguzo wana hisa kwako, unapowasaidia, unawasaidia jasho la wazazi wenu!
- Kama ktk wadogo zako kuna aliefeli shule, aliekosa fursa ya kusoma, aliekwama mahali, jua kukwama kwake ni kwa vile wewe ulishachota sehemu katika pato la familia, na sasa wazazi hawakuwa tena nguvu ile iliotumika wakati wa malezi yako!
Nawatakia jioni njema!