Wana CCM tusitafute mchawi wa kwanini tunendelea kupoteza. Waliotuponza ni hawa:
- Anna Makinda - Spika aliyehakikisha bunge linalinda masilahi ya serikali kwa kuzima hija za msingi na kuwaksirisha wapiga kura wetu.
- Wabunge wa vitu maalum wa CCM kwa kura zao za ndiyoooo kwa maamuzi yasiyona maslahi kwa taifa. zilikera sana wananchi.
- Taasisi ya rais na rais mwenyewe kwa kupuuza maazimio ya bunge yaliyomuhitaji katika utekelezaji wake.
- Samwel Sitta na team yake akina Lukuvi na Wasira kukanyaga maoni ya wananchi ya katiba mpya.
- Majina ya mfukoni ya ugombea urais
Kw kuongezea mambo yalionikera sana...
- Wapinzani kubaguliwa, kunyanyaswa na vyombo vya Dola kw uonevu.
- Vyombo vya Dola kushindwa kusimamia haki sawa kw kila mwanchi bila ubaguzi wa itikadi.
- Kashfa ya Tegeta Escrow na dharau kubwa ilionyeshwa ktk kuishughulikia.
- Sakata la Tokomeza, wananchi waliuawa bila sababu na madhara makubwa walipata bila sababu.
- Ujangili na usafarishaji wa Wanyama wetu kiharamia.
- Udhaifu mkubwa ambao haujawahi kutokea ktk Taifa letu ktk nafasi ya Hon PM, ni aibu na fedheha kubwa ambayo iliwaudhi sana Wananchi.
- Safari nyingi sana za nje zilizomhusisha Mkuu, wakati wananchi wakiweweseka na hali ngumu ya maisha, wakiteseka ktk umasikini mkubwa na kukosekana kwa huduma nzuri za kijamii.
- Ubaguzi mkubwa sana wa kiitikadi ktk TBC.
- Govt kudharau report ya CAG.
Wakati fedha zetu za umma zikiteketea bila Wahusika kuchukulia hatua za kufikishwa ktk vyombo vya Dola.
- PCCB kushindwa kuchukua hatua kw wale Mafisadi wakubwa.. Kwa kwel imekera sana.
- Govt kushindwa kununua vifaa muhimu vya vipimo, vitanda, mashuka na vifaa vingine kw ajili wagonjwa wetu ktk Govt Hospitals.
- Govt kushindwa kuwapatia wagonjwa wazee huduma bora zenye uhakika za matibabu.
- Elimu, badala ya kuwekeza ipasavyo na Govt kushiriki kikamilivu ktk Elimu yetu badala kufanya usanii wa kushusha viwango vya ufaulu, kw kweli imeumiza sana. Elimu yetu imepelekwa wapi?
- Gharama kubwa za masomo. Hakuna utaratibu wa kuweza kuwasaidia wanafunzi gharama za masomo - Masters, Phds...!
Etc. etc.