Wa enzi hizo mnayakumbuka haya?

Wa enzi hizo mnayakumbuka haya?

Ingawa mimi sio wa zamani kihiivyo lakini nimeshuhudia kaka zangu wakikamatwa eti kwa kosa la 'uzembe na uzuluraji' in mid-90s, mpaka leo sijawah elewa tafsiri ya lile kosa
 
enzi hizo kondom zilikua hazipatikani na zilikua zinaitwa DUREX. mtoto wa kiume hukosi kuugua gonorea japo mara tatu kwa mwaka
 
Na kukamatwa kwa kosa la uzembe na uzururaji[\b]


Haaa.....haa.....!!!! wazururaji Dar walikuwa wanapelekwa Geza ulole kulima. Mgambo wanaranda randa kila kona kusaka vijana vijiweni.
 
Wakati huo hata ukivaa kiatu kilichopanda juu mfano wa buti unavuliwa umevaa buti za polisi, nakumbuka miaka ya 90's watu wanapiga nyumba kufuli na kukimbia nyumbani kwa muda, kurudi jioniiii kisa bibi afya anapita
 
Enzi zile bia za halali zinapatikana DDC magomeni. DDC keko. DDC Kariakoo. DDC Mlimani park Urafiki na UFI Club. halafu kunywa bia ni kuanzia saa kumi.
kunywa bia enzi hizo ni ufahari sana
 
enzi zile Dar lazima upange chumba kwa mzaramo au mmanyema au mnanihii. kujenga nyumba utadhubutu bati au simenti utapata wapi.
 
Enzi hizo ukimuona mtu kavaa nguo nyekundu unatimua mbio eti mnyonya damu!

Enzi hizo ukisikia filimbi ya kushusha bendera ya taifa hata kama una kata gogo lazima usimame!
 
Back
Top Bottom