Wa Arusha kipindi cha jando kimeanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa Arusha kipindi cha jando kimeanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Dec 16, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Jana usiku muda wa saa 2:45 nikiwa narejea nyumbani maeneo ya Chini ya Mti karibu na lile kanisa la Nabii wa kiNigeria nilikumbana na msururu wa maandamano makubwa ya vijana wa kiArusha wakipelekwa jando [kuondoa suna bila ganzi nadumisha mila ile wengine wameshindwa].

  Wakuu najua JF wapo wanajamvi wenye kujua mila na tamaduni za kiMaasai/kiArusha chonde chonde naomba watumwagie mauzoefu ya hili zoezi zima tunajua vijana wanatahiriwa tunajua pia yapo mambo mengi ambayo hatuyajui eg ujasiri,kupewa majina ya marika ie Makaa,Seuri,Landizi na nk watueleze hayo majina yanapatinaje je taratibu za kuzuia maambukizi ya UKIMWI zinazingatiwa.....Je zoezi la kukeketa kina Dada wa kiArusha/Maasai wameacha limeachwa/limesitishwa siku hizi.

  Nawapenda sana waArusha/waMaasai wanadumisha mila katika mazingira ya dunia ya utandawazi.
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,178
  Likes Received: 10,517
  Trophy Points: 280
  mkuu wale jamaa wanaogopeshaga!! wakikuta wanaweza wakakuchapa viboko
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima tedo.

  Mkuu jana usiku ilibidi tupaki magari pembeni nyuma ya msafara waliwepo vijana wanne wameshika bendera nyekundu wakilazimisha magari yasipite bila utaratibu wao.Vijana waliokuwa wakiruka juu na kuimba nyimbo zinazoashiria wako tayari kukatwa biology yao bila ganzi sisi tukabaki wapole tukisubiri ruksa ya Morani.
   
 4. s

  sawabho JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 947
  Trophy Points: 280
  Hivi hii mila huwa ina wakati maalum wa kuitekeleza, maana kuna mtu aliniambia kule Kanda ya Ziwa kwa kina Mula inafanyika sasa hivi na wao wanatekeleza hata kwa Wadada.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya mambo muhimu kijana wa kiArusha akitoka jando lazima ayatimize.

  [1] Lazima ahame nyumbani kwa Baba/Mama yake.Hawezi kuishi nyumba moja na wazazi wake.Zamani walijenga nyumba kando ya nyumba ya wazazi.

  [2] Anakuwa tayari kuanzisha familia yake.Kijana akitoka jando anaweza kuoa na kuanza familia yake kwakuwa tayari kapata mafunzo namna ya kuishi na mke.

  [3] Anaweza kushiriki vikao vya ukoo kutoa maoni kwakuwa ana hesabika ni mtu mzima.Kijana ambaye ajaenda jando hawezi kuongea mbele ya wazee na ushauri/maoni yake yakakubalika.

  Tuomba wenye kujua zaidi waongezee,wasahihishe.Mila kama hizi hazitoi nafasi wala hazipokei masharti ya David Cameroun.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Sawabho.

  Mkuu nadhani hii shughuli inafanyika kila baada ya muda wa miaka kadhaa labda miwili,mitatu au minne ndiyo maana kila kipindi kina jina lake.Mfano kuna kundi wanaitwa Makaa wengine Seurii,wengine Landizi nadhani haijalishi umekwenda jando sehemu gani eg Pwani au Arusha au Kenya wote wanakuwa na jina moja kutegemea wakati gani umekwenda jando.

  WaArusha/waMaasai ni kabila unique sana wananifurahisha jinsi wanavyodumisha mila zao katika mazingira ya sasa.


   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ngongo heshima yako mkuu,

  Nasikia jando kwa kina dada haipo siku hizi, wameweza kuelewa athari zinazohusiana na tukio hilo.
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mzee wa Rula,

  Nadhani presha ya mashirika ya kutetea haki za kina Mama zimesaidia sana.Pamoja sana Mkuu.


   
 9. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ngongo hizi mila zimepitwa na wakati hazina maana tena ndani ya jamii ya kistaarabu.WaArusha na wamasaai kupitia jando wanaandaliwa kazi za ulinzi ambazo kipato chake ni hafifu sana.Dar ya miaka ya 80s kazi za ulinzi zilifanywa na wamakonde siku hizi kazi za ulinzi ni wamaasai watupu.   
 10. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wiki hii yote usiku nimewaona hata pale maeneo ya mianzini wakiwa na fimbo wanakimbia mchakamchaka! Sikujua ni kitu gani kumbe ndiyo wanaenda kutengeneza kisu. Asante kwa taarifa
   
 11. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kiafya ni hatari sana unaweza kupata maambukizi ya ukimwi iwapo hatua madhubuti hazitazingatiwa mfano kisu kimoja kitumike kwa mtu mmoja.

  Kitu kingine ni utaratibu wa kutairi.Mtu akitairiwa hospital nyama yote inaondolewa pia mshipa mkubwa wa damu unaokaa chini ya uume unakatwa na kushonwa kuzuia damu nyingi isitoke.Ukitairiwa kiArusha au kimasaai mshipa mkubwa haukatwi kwakuwa utaalamu wa kushona mshipa mkubwa unaokaa chini ya uume haupo.Ukitazama uume wa mmasai au mwarusha chini ya uume uliolala utaona nyama kubwa inanin'ginia nyama hiyo inajificha uume unaposimama.
   
 12. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanasababisha jam bila sababu wanatakiwa wakimbie mchaka mchaka maporini.

   
 13. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,467
  Trophy Points: 280
  asanteni waarusha endeleeni,endeleeni kudumisha mila.
   
Loading...