kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,425
- 13,935
Utaratibu wa kudahili wanafunzi kuingia vyuo vikuu nchini uendelee kufanywa kwa kutumia mtandao (CAS) kwakuwa umeonyesha ufanisi mkubwa sana katika kutoa fursa sawa kwa wanafunzi bila kuzingatia jinsia, dini, kabila, undugu, hadhi ya mtu kwenye jamii wala kipato cha familia ya mtoto. Mfumo ule wa zamani wa vyuo kuachiwa vitafute wanafunzi vyenyewe ulikuwa na mapungufu mengi sana hasa ya upendeleo wa wanafunzi wanaodahiliwa.
Enzi zile vyuo vilijaa watoto wenye makabila na dini za wamiliki na viongozi wa chuo husika, watoto wa viongozi wakubwa, watoto wa wenye mali, n.k. Ilikuwa vigumu sana watoto wa walima korosho kupata nafasi hasa kwenye vyuo vya watu binafsi au taasisi fulani zisizo za serikali. Watoto walikuwa wakidahiliwa kwa vimemo tu.
Mfumo wa utahiri kwa njia ya mtandao ni mzuri sana kama ukisimamiwa vizuri kuliko ule wa vyuo kuachwa kujitafutia wanafunzi wao