mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,036
Kwa mshangao mkubwa nimeona vyuo vikuu vikicheza rafu na kusababisha maumivu makubwa kwa wanafunzi. Nina uhakika na rafu hizo. Kuna jamaa Yangu alikuwa amechaguliwa vyuo vinne, na akaamua kuthibitisha chuo kimoja kilichokuwa cha kwanza kutoa kutoa jina lake. Alithibitisha kwa SMS na online mapema kabisa 07/10/2017.
Cha kushangaza ametokea kwenye orodha ya wanafunzi walioomba tena second round kwenye vyuo vingine viwili! Kati ya vyuo hivi viwili kimoja alikuwa amechaguliwa ile awamu ya kwanza lakini hakuthibitisha. Sasa wamedanganya kuwa aliomba tena chuo hicho second round kwa kozi hiyo hiyo waliyokuwa wamemchagua first round lakini hakuthibitisha! Hata mantiki ya rafu hiyo haina kichwa wala miguu.
Chuo cha pili wanachodai aliomba second round ukweli ni kwamba alikuwa ameomba first round chuo hicho na hawakumchagua katika hiyo first round japo ndiyo chuo alichokuwa anakipenda kwa kozi hiyo. Sasa wameamua kudanganya kuwa aliomba second round na wakamchagua kitu ambacho siyo kweli.
Athari ya rafu hizo kwa mwanafunzi ni kutokupangiwa mapema au kutokupangiwa kabisa mkopo maana inaonekana hatima yake bado haikajulikana hivyo TCU kushindwa kuwasilisha taarifa zake heslb kwa wakati.
Ninawataka TCU wawaagize viongozi wa vyuo hivi wawasilishe ushahidi kuthibitisha madai yao kuwa wanafunzi wameomba tena kudahiliwa kwao baada ya kuwa wamedahiliwa na kuthibitishwa kwenye vyuo vilivyowadahili awamu ya kwanza!
Vinginevyo hasara waliyosababisha jina lichelewe kupelekwa Heslb waifidie wao. Natoa siku tatu baada ya hapo nitátafuta msaada wa kisheria niwapeleke mahakamani!