SERIKALI imetoa waraka unaovielekeza vyuo vikuu vyote nchini, kuchelewa kuanza muhula wa masomo kwa mwezi mmoja, ili kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
................................
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, alisema vyuo hivyo vitafunguliwa kati ya Novemba 4 na 5.
Hata hivyo alisema hatua hiyo haitokani na uchaguzi na kwamba inatokana na mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na serikali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.
..............
.......................
"Tatizo kila kitu kinachofanywa sasa na serikali kinahusishwa na uchaguzi kwa sababu tu tunaelekea kwenye uchaguzi lakini hili la kufunguliwa kwa vyuo Novemba, halina uhusiano kabisa na uchaguzi,"alisisitiza Kawambwa.
........................
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Profesa Mayunga Nkunya, alithibitisha kupata taarifa kuhusu hatua hiyo.
Profesa Nkunya alisema, katika kipindi cha Oktoba, wanafunzi wengi watakuwa wakishughulia mikopo kutoka bodi ya mikopo na kwamba halitakuwa jambo zuri kazi hiyo isiingiliane na uchaguzi mkuu.