Habari za asubuhi wanajukwaa!
Jana nilienda Uwanja wa Taifa katika tamasha la Krismas. Sasa ikafika wakati nikataka kwenda haja jamani! Nikakutana na hali hii:
- Hakukuwa na maji kwenye vyoo
- Hakuna dust bin za kuwekea uchafu katika vyoo vya wanawake
- Kwa hiyo vyoo vilikuwa ni vichafu mno kiasi kwamba watu wengine wanakojoa chini tu
Kwa kweli hali ya vyoo uwanja wa Taifa ni mbaya mno!
Mi nilighairi kwa kweli ikabidi nivumilie tu mpaka wakati wa kutoka. Kuna watu waliokuwa hawawezi kujizuia wakijisaidia hivyo hivyo kwenye vyoo vichafu.
Ninaomba uongozi husika wa Uwanja wa Taifa washughulikie jambo hili mara moja kwani ni kero na linashusha hadhi ya huo uwanja!