Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,676
Mhariri wa Gazeti la "Telegraph" katika Tahariri yake leo ameitaka Serikali ya Uingereza kufikia kikomo katika kutoa misaada kwa nchi za Kiafrika kwani nyingi badala ya kutumia ktk maendeleo inatumia misaada hiyo ktk shughuli nyingine na huku nchi hizo zikiwa hazifuati mifumo ya "demokrasia na Utawala bora"
Time to end the foreign aid profligacy
Tories blow £200 million in foreign aid on corrupt Tanzania which held a RIGGED election
Britain under pressure to review £200 million aid for Tanzania after US cuts support
Hali hii inafungua ukurasa mpya wa "mgogoro wa diplomasia ya uchumi-Economic diplomacy" kati ya Tanzania na Mataifa ya Magharibi.Je matishio haya ya "vikwazo" vya misaada yanaiweka Tanzania katika mizania ipi ya kiuchumi ndani ya utawala wa miaka mitano wa JPM?Je tumejiandaa kujitegemea bila hawa "mabwana wakubwa?"...Hali hii ya vikwazo ina lolote nyuma ya pazia juu ya kubanwa kwa matakwa ya wakubwa hawa na misimamo ya uongozi wa JPM.Tunamsubiri Rais akitoka Chato kupumzika labda atakuwa na la kutuambia,maana wale wa umri wangu enzi hizo mkiona Mwalimu ameenda Butiama kupumzika ujue akirudi huku mjini basi anarudi na jambo la kutikisa dunia na jumuiya ya kimataifa.