PreGE2025 Vyombo vya Habari visitumike kudhoofisha vyama vya upinzani. Vitangulize weledi kwa maslahi ya umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,410
Reaction score
4,988
Katika siasa za Tanzania, vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuathiri mitazamo ya wananchi. CCM imekuwa na ushawishi mkubwa juu ya baadhi ya vyombo hivyo, hali inayodhoofisha upinzani. Kwa mfano, vyombo vingi vinatangaza mafanikio ya CCM huku vikifunika au kupotosha taarifa za wapinzani.

Matamko ya vyama vya upinzani mara nyingi hayapewi nafasi, au huonyeshwa kwa namna ya kubeza, mfano ni mgogoro unaoendelea sasa hivi CHADEMA baada ya kuibuka kundi linalojiita G-55.

Pia soma > Tundu Lissu: Vyombo vya Habari havitendi haki kwa Vyama vya upinzani, vyote vinakuwa vya CCM

Vyombo huru navyo hukumbwa na mashinikizo, kufungiwa au kutishiwa pale vinapotoa majukwaa kwa upinzani. Hili linazima uhuru wa habari na kuathiri demokrasia.

Tanzania inahitaji vyombo vya habari huru na visivyoegemea upande wowote. Wananchi wanastahili kupata taarifa kutoka pande zote ili kufanya maamuzi sahihi. Upendeleo wa vyombo vya habari haupaswi kuwa silaha ya kisiasa, bali zana ya kukuza uwazi na uwajibikaji.

Hali ya Vyombo vya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Kuna uhuru wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yao?



 
Legacy media zinapitwa na wakati, sikuhizi watu wana pay attention online medias sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…