Vyombo vya habari sasa mko huru, anikeni uchafu raia tupumue

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Kwa miaka kadhaa vyombo vya habari viliminywa mdomo na vikakubali kuminyika kiasi kwamba hata dira ya dunia ya kina Kikeke makeke yalipungua

Leo nimepata fursa ya kumsikiliza Esther Matiko, mbunge wa viti maalumu (kwa mujibu wa Spika)

Kwa asilimia kubwa mbunge huyo alikuwa akiongelea uzalilishaji unaofanywa na vyombo mbalimbali kiasi cha kuvunja haki za binadamu

Mfano ulionigusa ni kuhusu namna wafungwa na mahabusu wanavyokaguliwa gerezani

Haingii akilini mfungwa au mahabusu kuvuliwa nguo zote na kurukishwa kichura chura eti ku trace Kama ameficha kitu chochote sehemu za siri

Hebu piga picha Baba au Mama mtu mzima, anavuliwa nguo zote kisha kuruka kichura chura pengine mbele za watu rika ya mwanae eti kumkagua Kama ameficha kitu ukeni au njia ya haja kubwa

Taratibu Kama hizi ziliwekwa na wakoloni kwa malengo ya kumnyanyasa na kumdhalilisha mwafrika ili wao kujilinda na kulinda maslahi yao.

Ni ajabu hata baada ya ukoloni tumeendeleza taratibu zile zile za udhalilishaji.

Ni jambo la ajabu watu wanaenda gerezani na kurudi miaka yote hii lakini vyombo vya habari vimeshindwa kuyaweka hadharani ili jamii zipaze sauti

Mambo yakidhalimu yanapokaliwa kimya hakuna atakaye yarekebisha ila yakisemwa semwa hadharani na kujadiliwa kwa uwazi (Kama alivyofanya Matiko ambaye alijitolea mfano mwenyewe alipopelekwa segerea) ufumbuzi utapatikana tu.

Nitoe rai kwa vyombo vya habari, Kuna Mambo mengi sana ya kufanyia kazi kama haya kuliko kila siku kutulisha habari za ziara za viongozi na udaku wa kisiasa
 
Back
Top Bottom