Vyombo vingapi vinavyoisimamia Serikali?

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,525
2,000
Nisaidie kwahili,

Nimekuwa nikijiuliza Sana, ni vyombo vingapi humu nchini vinalojukumu la kuisimamia serikali?

Kwa ufahamu wangu, ni bunge la Jamhuri ndilo lenye wajibu huo, lakini ni miaka mingi sasa nimeona CCM nayo imekuwa na jukumu hilo, ukiuliza utajibiwa wanasimamia utekelezaji wa ilani ya chama.

Utawaona hawana tofauti na watendaji wa Serikali. Mfano mzuri hili la sakata la luku juzi. Shirika laweza omba msamaha
Serikali kuu CCM nayo imeomba msamaha.

Ipi Serikali na kipi chama?

Tumeona wakati wa katibu mkuu bashiru, maeneo mengi akihutubia taifa hususan kwenye migogoro akiwaagiza mawaziri wakuu wa mikoa na wilaya.

Mimi inanichanganya ipi Serikali na mkuu wa watendaji wa serikali ni nani?

Utaona Askari wetu wakitoa saluti ama kwa muenezi wa CCM au katibu mkuu.

Wajuzi nisaidie
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom