mara ya kwanza nilipoliona tatizo hili, sikuliona kwa mapana sana kwakuwa nilikuwa naamini waliofanya hivyo toka mwanzo walijua risk wanayochukua na niliamini walijipanga jinsi ya kukabiliana nayo. kumbe sivyo hivyo ,binadamu husahau na ndivyo kilivyotokea kwa wengi na matokeo yake ni maumivu na machungu mazito sana kwao na hasa wakikabiliwa na mzigo na uchungu mzito kwa yaliyotokea.
binafsi nauona upungufu kwa pande zote tatu serikali ambaye ni mdau mkubwa, muhusika na jamii kwa jumla ambyo ndio tuliotengeneza machungu yaha kwa kuwaelekeza wenzetu kuwa inawezekana fanya hivi au vile.
kuna hasara kubwa sana kwa hawa watu kwa yale yaliyotokea kwao na kwa wale waliokuwa wanawaudumia pia. mfano kwa daktari bingwa aliyefuzu vizuri kozi yake ya udaktari na amekuwa akiwaudumia vizuri watu wake na akiaminika akiwa na vyeti halali vya udaktari ila hana cheti cha form four, kumtoa huyu katika huduma ni hasara kubwa kwa taifa.
naweza kueleza na kutoa mifano mingi lakini ifike wakati nini kifanyike:-
- wale wenye taaluma wajitambue kuwa pamoja na mapungufu hayo wao wanauwezo na uzoefu mnzuri wa kufanya kazi hiyo na wajivunie kwa uwezo wao.
- jamii itambue mchango waliotoa katika mafanikio yao kama wataalamu. inasikitisha unakutana na mtaalamu wa kilimo na mifugo wa kata ambaye amekuwa akiwasaidia kwa kiasi kikubwa wanajamii lakini leo tunamsomea na kumwona hafai tukisahau tulivyokuwa tukimwamsha ahudumie ng'ombe wako wakizaa.
- serikali nafikiri bado inahitaji kuangalia upya ni kwa jinsi gani watu hawa wanaweza kutumika na sekta binafsi kwa kutoa vyeti vya kuwatambua kuwa ni watendaji wazuri ila hawakuweza kukidhi vigezo vya ajira serikalini.
- mwisho jamii haitakiwi kuwadharau na kuwanyanyapaa kupita kiasi kwa zaidi ya ugonjwa usio na jina wala tiba kwa kuwa bado tunawahitaji kwa maendeleo yetu.
- pia walioathilika wajikubali na wajipange na wapunguze maumivu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili. bado jamii inawahitaji na fursa bado zipo msiogope.