Vyeti vya ndoa hatuna

mhugo hantish

Senior Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
137
Reaction score
36
Mpaka sasa ninavyoandika thread hii naugua kwa maumivu makali sana juu ya nchi yangu Tanzania.
Issue yenyewe ni hii hapa...

Mimi nimeoa Nina mke mmoja tangu mwaka 2016 mwezi wa 10. Tulipotakiwa kutunukiwa vyeti/shahada za ndoa takatifu Mchungaji alituambia kwamba tusubiri kidogo vyeti tumeshaagiza na vitafika soon ndani ya muda wa mwezi mmoja.

Ni kweli tulisubiri. Lakini hadi kufika tar 18/2/2017 nilipoenda tena kumwulizia mchungaji wetu atupatie vyeti vyetu akatuambia kwamba hadi sasa bado hawajapewa toka wizarani. Na kwenye stock zao kama ofisi ya mchungaji zimeisha. Hadi leo nimeuliza lakini majibu ni yale yale na zaidi sana hata mchungaji nae anashindwa kufaham ni nini kinazuia vyeti vya ndoa kutolewa.

Swali langu kwa wizara husika ni hili.. Kipi kimepelekea tukose vyeti hadi leo hii? Je, Kuna uhakiki wa ndoa hewa(feki)?, Je, hamdhani ya kwamba kwa kukosa kwetu vyeti tunashindwa kutambulika kisheria kwamba Sisi ni wanandoa halali?

Je, kwa kukosa kwetu vyeti/shahada hamdhani ya kwamba tunanyimwa haki stahili anazopaswa kupatiwa kama mwanandoa halali? Na hii inakuhusu hasa wafanya kazi.
Je, ni kipi kimechelewesha ama kimekwamisha kutoa vyeti ambacho hakikustahili kutolewa ufafanuzi kwa raia wema wa Tanzania?

Na Je, ni nini mtazamo wenu kwa hili jambo?
Kama wahusika wataliona, nitafurahi sana na zaidi. Maana mimi ni muathirika wa jambo hili na sina utatuzi kwenye hili maana sijapata taarifa yoyote toka wizarani zaidi ya HATUJUI/HATUFAHAMU.

Mwinjilist.
 
NDIYO,
sio mara yake ya kwanza kufundisha ndoa, na hadi sasa ana umri wa kazi hiyo ambao kwa sasa anastahili kuretire kabisa Yaani.

Ndio anafungsha Ndoa je Kanisa lake limesajiliwa?, inaonekana kama alikuwa anagushi sasa upepo umebadirika anaogopa, vyeti vya Ndoa vipo vingi na issue ya Ndoa ni tofauti na vyeti vingine, hivyo vinasainiwa hapohapo wenye ndoa na mashahidi wao, iweje muoane na mkae miezi kadhaa bila vyeti, je mashahidi wakifa au kusafiri mbali nani atakusainia hicho cheti chako?
 
Yawezekana huyo mchungaji hana leseni ya kufungisha ndoa!!

Kama leseni anayo, kwanini haendi ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuchukua kitabu cha vyeti vya ndoa?? Ni nani aliyemwambia kuwa vitabu hivyo ni lazma akachukulie wizarani?

Kwa kuwa mchungaji hana leseni, kamwe hatoweza kupata kitabu cha vyeti, na kwa kuwa wewe unahitaji Cheti cha ndoa, nakushauri nenda ofisi ya DC, onana na DAS atakufungisha ndoa ya kiserikali na kisha utapewa cheti chako cha ndoa.
 
hatari sana,mwanandoa mmoja akifa hapo kwenye mambo ya mirathi itakuwa shida mtaonekana wazinzi tu hamjafunga ndoa
 
Huu ndio ushauri. Achana na ndoa feki hiyo kafunge ndoa upya achana na hiyo ya mchungaji. Kuna kanisa moja kubwa sana lina kawaida hiyo ya kulamba hela za vyeti wanatoa ahadi tu kama hizo za kihuni.
 
Makanisa mengi ya 'Vichochoroni' Wanafungisha ndoa paspo kutoa vyeti vya ndoa.

Nahisi mtoa mada ni mmojawapo wa kwenye hayo makanisa.
 
NDIYO,
sio mara yake ya kwanza kufundisha ndoa, na hadi sasa ana umri wa kazi hiyo ambao kwa sasa anastahili kuretire kabisa Yaani.

Umejaribu kuulizia hao waliofungia hapo wana vyeti vya ndoa?

Kama wote hamna basi Kanisa lenu na Mchungaji wenu hawajapewa idhini ya kufungisha ndoa.
 
ulifungia ndoa kanisa gani na linatambulika? na mchungaji wako anatambulika issue c anefungisha ndoa nyingi
 
Huu ndio ushauri. Achana na ndoa feki hiyo kafunge ndoa upya achana na hiyo ya mchungaji. Kuna kanisa moja kubwa sana lina kawaida hiyo ya kulamba hela za vyeti wanatoa ahadi tu kama hizo za kihuni.
Hatari sana!! Aende ofisi ya DC atalipia sh 50,000 kisha atafungishwa ndoa raha mustatehe!!!

Ila atasubiri siku 21 za kuitangaza ndoa hiyo
 
Umejaribu kuulizia hao waliofungia hapo wana vyeti vya ndoa?

Kama wote hamna basi Kanisa lenu na Mchungaji wenu hawajapewa idhini ya kufungisha ndoa.
NDIO.
Kwa mujibu wa nilivyo fuatilia kwa karibu, wadhamini wanavyo, kitabu cha orodha ya wanandoa walio kwisha funga ndoa zao siku za nyuma kabla yangu kinaonesha wanavyo.
 
Hatari sana!! Aende ofisi ya DC atalipia sh 50,000 kisha atafungishwa ndoa raha mustatehe!!!

Ila atasubiri siku 21 za kuitangaza ndoa hiyo
Hapana aiseh,
Siwezi fanya huo mchezo. This is unacceptable to me. But by any means I will fight until the success has come.
 
Huu ndio ushauri. Achana na ndoa feki hiyo kafunge ndoa upya achana na hiyo ya mchungaji. Kuna kanisa moja kubwa sana lina kawaida hiyo ya kulamba hela za vyeti wanatoa ahadi tu kama hizo za kihuni.
Si vibaya nikilitaja kanisa kwa nia njema. MAKANISA YA KKKT
 
Hapana aiseh,
Siwezi fanya huo mchezo. This is unacceptable to me. But by any means I will fight until the success has come.
Haya endelea kusubiri mchungaji aletewe vyeti vya ndoa toka wizarani mwinjilist!!!!!!
 
Siku unayofunga ndoa ndo siku unayosaini cheti cha ndoa pamoja na wale wasimamizi wawili kama mashahidi wa mbinguni na duniani . sasa wewe ulisaini kwenye nn? Kama hukusainishwa basi ndoa yako ni batili.....
 
Kwa taratibu za ndoa cheti unapewa hapohapo .si kwa waislanu wala wakristo hasa romani katoliki. Sijui huko kwenu mlisaini wapi baada ya kufungishwa ndoa .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…