Kuna ndg zangu wawili wamekumbwa nah ii ishu ya vyeti feki, hao jamaa walikuwa marafiki tangu wapo shule ya msingi Fulani hivi na baadae mpaka walipochaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari huko mkoani urafiki wao bado uliendelea kudumu na ikawa mpaka wazazi wao wanajua kwamba “huyu motto wangu rafiki yake mkubwa ni Fulani motto wa mzee Fulani” mpaka ikafikia kipindi familia ya A inapeleka mahindi au maboga kwa familia ya B kipindi cha mavuno.
Hakika urafiki wao huo uliendelea kudumu mpaka walipohitimu elimu yao ya Sekondari lakini kwa bahati mbaya huyu mwanafunzi A akapata alama za daraja la 4 la mwisho (tunaita Four chafu) na Yule mwingine B akapata daraja la 3 lakini hakuchaguliwa na masomo ya kidato cha 5&6, ila kwa bahati mzuri Yule B alikuwa na ndugu zake hapa Dar wenye uwezo wa kipesa hivyo akaja mjini hapa kujiunga na elimu ya kidato cha 5&6 shule ya Sekondari Jitegemee na wakati huo huo Yule rafiki yake aliyepo kijijini akaomba nafasi ya kwenda kusomea Ualimu kutumia cheti cha rafiki aliyepo Dar na akapata nafasi chuo cha Ualimu Vikindu. Wakawa wanatumia cheti kimoja lakini mmoja wapo akawa anatumia “middle name” kwenye majina yake lakini cheti kimoja mmoja yupo VIKINDU na mwingine JITEGEMEE.
Baada miaka miwili kupita Yule wa Jitegmee akawa amemaliza masomo ya kidato cha 5&6 na Yule wa Vikindu akawa amemaliza masomo ya Ualimu, Yule wa Vikindu akapata kazi mkoa wa pwani na Yule wa Jitegemee (mwenye cheti orijino) akapata bahati la kujiunga chuo kikuu cha kwanza kwa ubora Tanzania namaanisha UDSM akisomea uchumi.
Yule mwalimu akaanza kumpa kampani ndogo ndogo jamaa wa UDSM na enzi zile pesa za chakula zinachelewa basi ikawa jamaa anamtoa toa mwisho wa mwezi ukifika, Yule jamaa wa UDSM akapata demu mkali sana ila hakuwa mwanachuo na akamtambulisha mpaka kwa rafiki yake Yule Mwalimu wakawa wanafahamiana na ikafikia kipindi Yule “demu” anaenda kwa mwalimu si unajua alikuwa amepangiwa mkoa wa pwani wilaya flani iliyopo jirani na DAR. Jamaa amemaliza chuo halafu yupo kitaa hata ile ya boom hana anahangaika na bahasha apate kazi Yule mwalimu akatumia mwanya huo kumchukua demu wa rafiki na akamuoa kabisa ndoa ya Kiislamu tena kwa siri hata rafiki yake hakujua,
Jamaa Yule ambaye alimaliza UDSM aliposikia kuwa Yule mpenzi wake ameolewa na rafiki wa tangu primary alihuzunika sana ila kama mwanaume akapiga moyo konde na maisha yakaendeea kama kawaida, Yule jamaa akapata intern FINCA na baadae akaajiriwa WIZARA moja hivi inayohusisha kazi na Ajira na baadae ofisi ya Waziri Mkuu, ila kimbembe kimeibuka baada ya Bodi ya Mikopo kuanza kukata ile asilimia yao na sijui ilikuwaje wakaanza kukata kwenye mshahara wa mwalimu ambaye kimsingi hakusoma chuo cha Elimu ya Juu, akaanza kuwatumia marafiki wa jamaa wa UDSM wakamuambie arekebishe jamaa akasema ye hawezi kama vipi aende mwenyewe na sasa hivi ishu ya vyeti feki mwalimu anamuambia Yule aliyepo ofisi ya waziri mkuu arekebishe mambo jamaa yupo kimya.
Je, ikigundulika Yule mweye cheti orijino atasalimika..? ma yeye alitoa cheti chake kwa ridhaa huku akijua kosa kisheria..!