Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,324
- 152,136
Moja ya jukumu la vyama vya wafanyakazi ni kutetea maslahi na luhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
Hata hivyo,tangu awamu hii imeingia madarakani,kuna mambo yamefanyika ambayo kwa namna moja au nyingine bila shaka yatakuwa yameathiri watumishi wa umma.
Hivi sasa tunaona kila mtu amekuwa na mamlaka ya kuagiza watumishi wa umma wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi jambo ambalo hata mh.Lissu alihoji ndani ya Bunge lakini vyama hivi viko kimya!
Kwa mfano leo hii nimeona kupitia taarifa ya habari ya Star tv ya saa 4 asubuhi,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,bwana Stephen Kabwe akiagiza watumishi kadha wa Halmashauri wasimamishwe kazi katika mkutano wa hadhara uliohusu maswala ya wakulima na wafugaji.
Pia, tumeshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam,bwana Paul Makonda akiagiza watendaji wa Halmashauri za Jiji la Dar-es-salaam wasaini mikataba maalumu kuhusiana na swala la kudhibiti watumishi hewa.Nia ni nzuri lakini utaratibu ule ulikuwa halali?
Hiyo ni mifano michache tu miongoni mwa mingi tulioshuhudia.Pamoja na nia njema ambayo inaweza kuwepo, swali ni je,taratibu zinafuatwa?Ni kweli Wakuu wa Mikoa wana madaraka hayo?
Kinachonishangaza ni ukimya wa vyama vya wafanyakazi,vyama ambayo watumishi hukatwa mishahara hayo ili kuviendesha.Je,ni kweli vyama hivi havijaona hata jambo moja la kukemea?Vyama hivi vinasubiri watu wafukuzwe kazi ndio vijitokeze hadharani?
Mwaka huu serikali imepunguza PAYE kufikia single digit.Ni jamba jema na la kupongeza.Lakini mwaka huu kuna nyongeza ya mshahara iliyotangazwa rasimi na waziri husika?Vyma vya wafanyakazi vimehoji juu ya jambo hili?
Kuna taarifa zisizo rasimi kuwa kuna mpango wa kupunguza mishahara ya baadhi ya wafanyakazi ili kuleta uwiano.Je,jambo hili ni sahihi?Kama ni kuleta uwiano,kwanini iwe ni kwa kupunguza na si kuongeza mishahara ya watumishi wanaolipwa mishahara midogi?Sheria za utumishi zinaruhusu kupunguza mshahara wa mtu?Vyama hivi vya wafanyakazi vimewahi, hata kuhoji jambo hili?Je,vinasubiri migogoro itokee kati ya mwajiri na mtumishi ndio vianze kujitokeza kwenye vyombo vya habari na matamko ya hapa na pale?
Kuna hili swala la kuunganisha baadhi ya Idara na Taasisi za Umma zinazofanya kazi zinazofafana. Je,vyama hivi vimeshirikishwa?Vinajua nini kinaendelea kuhusu zoezi hili?
Wahusika timizeni wajibu wenu kama kazi imewashinda muwapishe wanaoweza.