Vyama vya Upinzani Tanzania ni Mfu au"Ghani" za Bi Kidude

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,714
2,000
Uhai wa vyama vikuu vya upinzani Tanzania - Chadema na CUF,kisiasa za kimambo leo uko ICU au mahatuti. Haieleweki kama viongozi wao wakuu ni wafu wa kisiasa au wachumia matumbo yao - wanaendelea kuimba ngonjera za mipasho ya Bi Kidude
Chadema
Lowassa anasema anafanya siasa za muono wa kimataifa.Katika kuwapumbaza wafuasi wake, amesema katika kuwatakia heri za mwaka mpya " Chadema kila watakachogusa kitakuwa dhahabu" Hizi ni Ghani za Bi Kidude - muhogo wa Jan'gombe utauramba mwiko!

CUF
Maalim Seif anasema, huku mapovu ya kimtoka, kuwa Serikali ya CCM Zanzibar haitasimama,haitadumu na itasambaratika muda si mrefu.CCM inaendelea kupeta, uchumi umeimarika(?)na makusanyo ya mapato kuwa maradufu. Wana CUF wao wanarambishwa asali kwa kuambiwa "wakae mkao wa kula na watembee vifua mbele." Vifua sasa vimebaki mbavu tupu hoi bin taaban. Maalim Seif anasubiri malaika kushushwa kutoka mbinguni kuja kumkabidhi ushindi wake ulioporwa. Ghani za Bi Kidude

Viongozi hawa hawawezi kuwatoa Watanzani "out of Bondage" Ni bora tendelee kumsujudia kafiri tupate mradi wetu.

Hongera na pongezi za dhati tuwape vyama vya Upinzani DRC waliosimama kidete kwa hali zote kuhakikisha hawayumbishwi, kusalitiana na kurudi nyuma katika kudai haki na misingi ya Katiba demokrasia inaheshimiwa na kukataa kuongeza "akina Nkurunziza" wengine katiko eneo hili

Heko kwa Wapinzani wa DRC na ZIIIII kwa wapinzani wa Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom