Vyama vya upinzani havijiamini

Vyama vya upinzani havijiamini

cardiologue

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
351
Reaction score
90
CCM inazidi kuchoka, hakuna chama cha upinzani kilicho tayari mpaka sasa kushika madaraka.Hii ni kutokana na aina ya siasa tunazoshuhudia kila leo.

0Kama wapinzani wanadhani kuwa ACT-Wazalendo ni janja ya CCM kupunguza kura za upinzani, kwanini wapinzani hao hao waliwafukuza viongozi wakuu wa ACT-Wazalendo kutoka vyama vyao vya awali?

Au nao ni matawi ya CCM ili kuvurugana wao kwa wao?Kama ni kuhofia nguvu ya ZZK ndani ya ACT-Wazalendo, kwanini hawakufuta kesi mahakamani ili kuja kunusuru kura za upinzani kugawanyika?

Ile dhana kuwa ACT-Wazalendo itapunguza kura, kwanini ni ACT-Wazalendo tu? Kama lengo ni kuitoa CCM madarakani, kwanini kila mtu asipigane kivyake mwisho wa siku tusubiri masanduku ya kura yaamue?

Nionavyo mimi vyama vya upinzani havijiamini.
 
Vinajiamini ila havina uwezo, ni dhaifu na hatuvitaki
 
Hata wewe pia hujamini, ACT ni Zitto na Zitto ni ACT siku Zitto akifa na ACT itakuwa imekufa.
 
Back
Top Bottom