herzegovina
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 3,129
- 4,712
Kwa lugha inayoeleweka kabisa ni kuwa nchi hii haikuundwa kuja kuwa nchi ya vyama vingi. Ilibidi tuigize kama tuna vyama vingi ili kuepuka "kibano" tulichokuwa tunakabiliana nacho kipindi hicho kutoka kwa mabeberu. Hata vyama vingi vilipoanzishwa Mali nyingi sana ziliekezwa kwa Chama Tawala.
Leo miaka 28, baada ya mfumo wa vyama vingi bado wapinzani wanaonekana kama maadui wa nchi. Wanaonewa, wananyanyaswa, wanafanyiwa kila hila. Sababu ni moja tu, "mifumo yote" inaamini na ina uhakika kuwa hawawezi kushika dola.
Vyombo vya habari havirushi mikutano, Polisi wanawatisha na kuwakamata, huko NEC ndio usiseme maana hata aibu hawana. Mnajua kwanini wanawafanyia yote haya? Ni kwa kuwa wanajua hamuwezi kuwa mabosi wao.
Katika hali ya usawa wa kidemokrasia, wagombea wowote wale wangekuwa wanaheshimika. Polisi asingemu-harass mgombea ubunge kwa kuwa anajua kuna uwezekano wa mgombea yule kuwa Waziri wa mambo ya ndani. Vyombo vingewaheshimu wagombea Urais kwa kuwa yoyote Kati Yao anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu n.k
Je, mfanye nini? Kwa kuwa imeshaonekana dhahiri kuwa hamthaminiwi na hamuwezi kushika dola hata iweje bali mnatumika tu kuuonyesha ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi, basi ni vyema baada ya uchaguzi huu mkafanya MAAMUZI magumu. Either ni wapinzani wote kwa pamoja kwenda kufuta vyama vyao kwa msajili (kwa njia yoyote ile) au wapinzani wote kwa pamoja kujiunga CCM ili vyama vya upinzani vikose hata kiongozi mmoja kuanzia ngazi ya taifa hadi mtaa hivyo vifutike automatically.
Kwa kufanya hivi CCM itabaki peke yake hivyo basi ile "hadaa" kwa ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi itakuwa imefikia mwisho. Nadhani yanayoendelea yanamulikwa hivyo kama kuna "kibano" kingine watatupa basi na iwe hivyo ili tutakaporudi kwenye suala la vyama vingi basi sasa iwe ni vyama vingi katika uhalisia.
Wapinzani mnatumika bila nyinyi wenyewe kujijua. Ifike mwisho.