Vyama vya kikanda vyuoni

Vyama vya kikanda vyuoni

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,104
Reaction score
1,924
Hivi vyama msingi wake ni kushirikiana tu,au kuna nini nyuma
ya pazia? maana kama ni kusaidiana,watanzania ni wamoja Tangu uhuru,iweje kuwe na vyama vya ukanda?
 
Mbn hujaelezea ueleweke?vyama gani?chuo gn? Na ikoje?
Ndg yangu labda sema unaitaji msaada wa kueleweshwa,,kuna vyama vya watu wa Kanda ya kusini,Kagera,Kazikazini,Tanga,yaan ni kero tu
 
Hahaha kuna makabila kila mwanafamilia ana chama chake, usiogope ndio walivyo.
 
Acha wivu wa kijinga. Mbona mtaani huku kuna vyama vya makabila aisee. Utakuta chama cha watu wa Singida, Moshi, Mbeya etc. Na wana michango kila mwezi. Usiwe chongo kuangalia tuu chuoni.
 
Lengo la hivyo vyama mtaani ni nini? hampati huduma gani mpaka mjionyeshe kuwa nyie ni watu wa sehemu flan?
 
Lengo la vyama ni kuinuana uchumi lakin pia kusaidia maendeleo ya kule mnakotoka, kusaidiana katika mambo ya kijamii kama misiba, nk ukipata msiba na ni wa kusafirisha ndo utaelewa maana ya hivi vyama lakin kama haujapata kadhia kama hiyo ni ngumu kuelewa
 
Afadhali mkuu umejibu vyema. Hawa vijana wanaokua bado hawajajua maisha ya uswazi yakoje. Kijana katoka zake form six mambo fresh kwao kajiunga chuo anapata boom na visimu vya kupyatila headphone masikioni hawawezi kuelewa haya mambo. Sisi tulioko uswazi tunajua. nilishawahi kupatwa na matatizo ya msiba yaani kama siyo jamii kunibeba sijui ningefanyaje maana nilikuwa ugenini mikoa ya watu.
 
Mleta mada kama anataka kujua haya mambo, akatafute kitabu cha historia kilichoandikwa na John Iliffe, A Modern History of Tanganyika, ameelezea historia ya vikundi hivi kuanzishwa hapa Dar es Salaam miaka hiyo wakati wa ukoloni, na vimesurvive mpaka leo
 
Afadhali mkuu umejibu vyema. Hawa vijana wanaokua bado hawajajua maisha ya uswazi yakoje. Kijana katoka zake form six mambo fresh kwao kajiunga chuo anapata boom na visimu vya kupyatila headphone masikioni hawawezi kuelewa haya mambo. Sisi tulioko uswazi tunajua. nilishawahi kupatwa na matatizo ya msiba yaani kama siyo jamii kunibeba sijui ningefanyaje maana nilikuwa ugenini mikoa ya watu.
Wanawaza ujinga ujinga tu, hawajakutana na matatizo
 
Hivi vyama msingi wake ni kushirikiana tu,au kuna nini nyuma
ya pazia? maana kama ni kusaidiana,watanzania ni wamoja Tangu uhuru,iweje kuwe na vyama vya ukanda?
Ni kutafta wachumba wa kabila moja na kuendeleza ukabila na ubaguzi tuu. Ni moja ya ujinga mkubwa sana unaoendekezwa na vyuo. Nyerere angekuwepo wote wangechapwa viboko...
 
Back
Top Bottom