Vyama vikubwa vya kisiasa tanzania

Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,476
4,250
Ndugu zanguni,
Nilikuwa nimelala na ndo nimeamka!
Sasa hivi, wagombea wetu wa uchaguzi ujao watapita kwa chama lipi? cha-CCM, cha-DEMA, Cha-NCCR, cha-CUF ama ?? nadhani sasa hivi vyama vikuu vipya ni WAKATOLIKI na SHURA YA WAISLAMU. Sasa ngoma iliyopo ni je vyama hivi vitawasupoti akina nani/wagombea gani???

Tuombe sana,
Amani.
 
Last edited:
CCM itavuna inachopanda ,maana wameshindwa kusimamia uchaguzi wa haki na kuleta uchaguzi wa mafisadi ,wakiambiwa wabadilishe KATIBA hawataki ,wakiambiwa wabadilishe TUME ya Uchaguzi hawataki ,wakiambiwa waendeshe uchaguzi wa Haki pia hawataki ,sasa wanalolitaka litokee katika nchi hii watalipata na wao walioko madarakani ndio watakao beba lawama na pindipo yakitokea ya kutokea wao ndio watakaosakwa kama Omar Albashir.
 
Vyama vikubwa vya siasa ni CCM na Chadema, vingine vikiongozwa na CUF ni vya kidini.
Muhimu:
CUF ni chama cha kiislamu
 
Wakatoliki na Shura ya Maimamu sio vyama vya siasa. Hawa wametoka mwongozo kwa waumini wao ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi ili wasije wakawachagua viongozi wasio waadilifu. Sijasoma waraka wa hawa Maimamu ila nasikia haujakaa vizuri. Kwa upande mwingine sio suala la chama. Mtu atakachaguliwa kwa uwezo wake na uadilifu bila kujali anatoka chama gani, dini gani na kabila gani.
 
Back
Top Bottom