MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Hivi vyakula nafaka aina zote kwa sasa bei iko juu inayoendea kua mara mbili ya bei ya mwaka Jana, hivi ni kweli hakuna njaa au ni mabadiliko ya mfumo wa msisha? Mfano kilo moja ya unga wa mahindi kwa sasa ni 1600 hapa mkoani Arusha, hiki ni kiashiria cha nini? hii ni January lakini kufikia Aprili hali itakuaje?
Nakumbuka Mh Rais aliwahi kuwaambia wakulima wauze vyakula kwa bei waitakayo, kwahiyo inawezekana kabisa hata udhibiti wa bei hizi inaweza kua ni tatizo kwa sababu ya kauli kutoka juu! Kuwaambia wakulima wauze mazao kwa bei watakazo wao ni sawa na kuwapa rungu kuwaponda walaji hasa zile familia zinazoshindia mlo moja kwa siku.
Kiuhalisia hali si salama kabisa upande wa vyakula kwa sasa, bei zinapaaa kwa kasi na hakuna udhibiti wowote Kama ilivyokua kwenye sukari na wananchi hawana cha kusema.Sio wakulima kuuza vyakula kwa bei watakazo tu bali ni uhaba wa bidhaa hizo, hatuwezi kuendelea kusema tuna Chakula cha kutosha huko kumbe tuapigia mahesabu ya bidhaa za wafanyabiashara bila hata udhibiti wa bai zake.
Sisi makabwela huku mitaani hatuna uwezo wa kusema kwamba kuna njaa kwa sababu ni kauli ya kuudhi ila lazima tuseme ukweli kua hali ni ngumu sana huku. Mtu unaweza kusema kua huna maradhi flani lakini unashindwa hata kutembea watu wanaweza kukushangaa.Hivyo sisi huku mtaami hali halisi ya vyakula Mungu anaijua.