Vurugu za Umeya Dar: Polisi wazingira nyumba ya Halima Mdee kumkamata. Ajisalimisha!

Oct 7, 2015
86
108
Polisi wamekwenda 'kuzingira' nyumba ya Halima Mdee wakitaka kumkamata kumpeleka central police kwa issue inayohusu uchaguzi wa umeya Jiji la Dar es Salaam.

==========
UPDATES:

Mbunge wa Kawe Halima Mdee amejisalimisha mwenyewe Polisi kutokana na sakata la umeya wa jiji la Dar es Salaam, ambapo muda mfupi baadae jeshi la polisi lilizingira nyumba yake kwa lengo la kumkamata.

Halima amewasili akiwa na wanasheria wake baada ya kupata taarifa kuwa polisi wanamtafuta kwa udi na uvumba wakimuhusisha na "vurugu" zilizotokea wakati uchaguzi wa Meya wa Jiji
 
VURUGU ZA UMEYA: Polisi wazingira nyumba ya Mbunge wa Kawe H. Mdee ili kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano,itakumbukwa kuwa katika mkutano na waandishi wa habari Kamanda Sirro alisema ni lazima wote walioleta "vurugu" katika uchaguzi ule watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola
image.jpeg
 
Waambie kuwa ni Wapuuzi kuliko upuuzi wenyewe.... kwanini wasiwakamate wale wapuuzi wa CCM waliogoma kuingia kwenye uchaguzi? waambie watumie vichwa vya ju kufikiri sio nanihiii
 
Sasa mtu kama Halima ni wakukamatwa wakati wangeweza kumpigia simu aende mwenyewe? Baads ya Siro kukabidhiwa kanda nilitegemea maigizo ya Kova yangeisha
 
Kwa ninavyoelewa aliyepigina na aliyepigwa wote wameleta vurugu. Mbona hawafuati sheria ktk kukamata? Kuna agenda ya siri. Huo uonevu una mwisho.
 
Eeeeee Mwenyezi Mungu bora ushushe tu gharika tufe kuliko haya manyanyaso tunayopata toka ccm kupitia vyombo vyake vya dola
 
Back
Top Bottom